Monday, November 12, 2012

WAIMBAJI NA WAIGIZAJI WAZIDI KUOKOKA


Dotnata Posh.
Hizi ni siku za mwisho na YESU yu karibu sana kuja kuchukua au kunyakua kanisa lake. Moja wapo ya ishara kuu ya siku za mwisho iliyonenwa na Yesu mwenyewe katika kitabu cha Mathayo ni Kwamba Injili itahubiriwa kwa kila kiumbe ndipo ule mwisho utakuja. Hivi karibuni kumetokea wimbi kubwa la waimbaji na waigizaji nje ya kanisa wa ndani na nje ya nchi kuamua kuachana na mambo au maisha ya dhambi waliyokuwa wakiishi na kuamua kumrudia MUNGU wao na kujiunga na makanisani.

Hilo limedhihirika nchini kwa waimbaji na wanamuziki kumrudia muumba wao kama ilivyo huko nchini Malawi ambako tunaambiwa waimbaji wengi wameamua kurejea kanisani kumuimbia Mungu kama lilivyoripoti gazeti la Nyasa Times kwamba waimbaji muziki zaidi ya watano wameokoka na kuamua kumwimbia Mungu wao huku wengine wakianzisha na bendi zao kabisa za gospel.

Kati ya waimbaji hao maarufu waliokoka ni pamoja na Sam Sambo, Mlaka Maliro, Phungu Joseph Nkasa, Bon Kavalasanza, Evans Meleka na wengine, ambapo wengi waliozungumza na gazeti hilo wameeleza ninamna gani walivyokutana na Mungu nakuamua kumkabidhi maisha yao.

Kwa upande wa Tanzania waimbaji na waigizaji ambao wameamua kumkabidhi maisha Yesu ni pamoja na Dotnata Posh ambaye ameshatoa wimbo wa gospel na sasa yupo katika masomo ya biblia na kuahidi kufungua kanisa pia aliweka bayana kwamba anampango wa kuwachukua mwimbaji Rehema Chalamila(Ray C), Aisha Madinda ambao amesema wameokoka kwasasa.
Vincent Kigosi (Ray)

Wengine ni Stara Thomas ambaye pia tayari ametoa album ya gospel, wengine ambao walitangaza kuokoka miaka ya karibuni ni pamoja Vincent Kigosi (Ray), Mwanaidi Suka ( Mainda), K- Bazil ambaye kwasasa yupo mkoani Iringa kama mchungaji( kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata), Emanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji ambaye ndoto yake ya kuwa mchungaji amekwishaianza kwa kuhubiri katika mikutano mbalimbali pamoja na wengine wengi.
Stara Thomas.

Swali ni kwa wale waliopo kanisani je wanapokeaje taarifa hizi za wapendwa hawa, je wanachukua jukumu la kuwaombea ama wanachukua jukumu la kuwahukumu?.. ni wajibu wa kanisa sasa kuwalea watu hawa ili wajifunze na waishi maisha ya kumpendeza Mungu.Ni maombi yangu kwamba Mungu wa mbinguni awasaidie wailinde imani ya kweli waliyoipokea hata siku ajapo mwana wa adamu tukamlaki sote mawinguni Amen.
Mwanaidi Suka (Mainda).




Kashumba Bazil (K-Bazil)
Aisha Madinda.                                                                                                                           



No comments:

Post a Comment