Askofu mpya wa Anglikana Justin Welby (kulia) |
Aliyetangazwa kuwa askofu mkuu wa kanisa
Anglikana Cantebery na ambaye amethibitishwa hii leo, Justin Welby
amesema ameshangazwa sana na wadhifa aliopewa wa kuliongoza kanisa hilo.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu
Justin Welby ambaye ni askofu wa Durham, alielezea msimamo wake wa
kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake kama maaskofu.Welby aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta , anaonekana kama mhafidhina kwa mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea upande wa kiivanjelisti. Ataanza kazi yake mwezi Machi mwaka ujao baada ya Askfo mkuu Rowan Williams kuachia ngazi.
Baada ya uteuzi wa Askofu mkuu Justin Welby kuwa mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo wamezungumzia uteuzi huo.
Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Nigeria, Nichola Okoh, ameimbia BBC kuwa uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja usitetewe na Kanisa.
No comments:
Post a Comment