Askofu wa Durham, Justin Welby, ambaye pia
ni mfanyakazi wa zamani katika sekta ya mafuta, anatarajiwa kutajwa
kama askofu mpya wa Canterbury.
Askofu Justin Welby |
Duru kutoka makao makuu ya waziri mkuu nchini humo, zinasema kuwa askofu huyo atatangazwa rasmi siku ya Ijumaa.
Mnamo Jumanne, wadadisi waliwacha kubahatisha kuhusu nani atachukua wadhifa huo baada ya watu wengi kutabiri kuwa yeye ndiye atachukua nafasi ya Rowan Williams
Jarida la Daily Telegraph, lilinukuu kuwa Askofu Welby amekubali kuchukua wadhifa huo ingawa kwa sasa hangeweza kutoa tamko lolote kuhusu udadisi juu yake.
Askofu Welby alisomea chuo kikuu cha Cambridge na kisha kufanya kazi katika sekta ya mafuta kwa miaka kumi na moja kabla ya kusomea dini ambapo baadaye alitawazwa mwaka 1992.
No comments:
Post a Comment