Saturday, November 10, 2012

Baada ya matokeo:Amerika imeacha somo gani kwa wakristo?

Rais Barack Obama


Uchaguzi wa Marekani 2012 umemalizika, zaidi ya waamerika 100 millioni walishiriki katika zoezi hili kubwa la kidemokrasia wakitimiza matakwa ya upigaji kura. Hata wakati  zaoezi la kuhesabu halijaisha na michakato mingine ya kiufundi haijakamilika, mwonekano wa ujumla wa uchaguzi ulikuwa wazi, na matokea ya uchaguzi huu kwa hakika ni makubwa na hayatasahaulika kiurahisi miongoni mwa watu wote duniani.
Mambo kadhaa yamejitokeza mara baada ya uchaguzi huu na wakristo kote duniani hatunabudi kuyatafakari kwa kina na kwa makini.

USHINDI WA KUTULIZA
Kwanza, ni lazima tutambue kwamba Rais Barack Obama ameshinda ushindi wa wazi na ulioleta ushwari wa utulivu katika taifa, kura ziliongezeka kwa kasi kufikia zaidi ya 300 kabla ya usiku wa manane. Kinyume cha matarajio ya wengi, ambapo uchaguzi wa 2008 Rais aliunganisha nguvu nyingi pamoja. Kura nyingi kutoka miongoni mwa vijana wa kiamerika, Waafrika-Waamerika, Wahispania, na majimbo mengine muhimu. Mara matokeo ya uchaguzi yalipoanza kutangazwa kimajimbo, ushindi wa Obama ulionekana kiurahi na kwa uwazi kabisa.
Rais Obama akiwa na familia yake baada ya kushinda uchaguzi

Barack Obama aliepuka aibu ya uchanguzi ambayo pia angeshinda kwa kura nyingi. Asili ya kuyatuliza mambo kwa ushindi alioupata umeliokoa taifa na maumivu makali ambayo lingeyapata kwa chaguzi na pointi elfu mbili (2000)  kwa kuleta uamsho na ari mpya katika chama chake. Mambo mengine pia yamekuwa wazi. Uchaguzi umemrudishia na kura zimeonyesha kwamba msimamo wa Rais Obama juu ya swala la ndoa za jinsi moja (same-sex marriage) hauja mgharimu chochote. Hii labda umewashangaza watu wote waliokuwa na misimamo tofauti na wa Rais mteule.
Wakristo sasa hawana budi kumwombea Rais mteule wa taifa kubwa hili. Kama mtume Paulo anavyoelekeza, “Basi kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utaua wote na ustahivu” (1 Tim 2:1-2). Ni lazima tumwombee Rais. Hatuna budi kumwombea afya njema pamoja na familia yake kwa ajili ya stamina na tabia nzuri katika kutimiza majukumu yake ya kila siku. Ni lazima pia tuombee timu nzima ya uongozi ili iweze kuonyesha na kutenda vyema hatimaye iweze kukumbukwa kama ni moja ya timu bora katika historia ya taifa hili.
Wote tunahusika kwa karibu sana. Ni lazima tumwombe MUNGU ili augeuze moyo wa Rais  Obama katika kushughulikia mambo mazito ya taifa hili, hasa kusimamia utakatifu kuanzia maswala ya utoaji mimba mpaka maswala ya heshima ya ndoa yanayosumbua watu wengi hivi sasa. Ni lazima tuende kinyume na kila hali ya uchafu hasa mikakati mbalimbali aliyonayo katika swala zima la njia za kuzuia mimba zilizo kinyume na maadili ya uhuru wa Kidini. Tukiangalia hali yake ya uongozi kwa muhula wake wa kwanza Ikulu (White House), ni lazima tufanye mapema hasa kwa muhula huu wa pili, tukijua kwamba Rais huyu hata shiriki tena katika uchaguzi kwa mujibu wa sheria za Marekani.
Kama Rais alivyodhibitisha katika hotuba yake mara baada ya kuchaguliwa mara ya pili kuwa Rais wa Taifa la Marekani, kwamba Taifa letu linakabiliwa na changamoto kubwa. Hivyo hatunabudi kumwombea Rais ili aongoze katika roho ya umoja wa kitaifa na kuheshimiana, Waamerika wawe wamoja katika kutatua matatizo yao kwa umoja. Majukumu mazito sasa yako begani mwake. Ameshinda mara ya pili kwenda ikulu, sasa ni lazima aongoze kwa haki.
Rais Barack Obama akiwa na makamu wake wa urais pamoja na wake zao

Uchaguzi uliligawa taifa
Asubuhi ilipofika, uchaguzi wa mwaka 2012 ulikuwa hautabiriki kwa vile kura na matokeo yalikaribiana sana kati ya chaguzi zote zilizowahi kufanyika katika historia ya Amerika, saa nane usiku., kura 240,000 tu kati ya zaidi ya 103 millioni zilizopigwa ziliwatenganisha Rais Obama na Govana. Mitt Romney. Tofauti ya  .3% imeufanya uchaguzi huu kuwa wa tatu kwa wagombea kuwa na matokea yaliyokaribiana sana katika historia ya Amerika, akishindwa kwa kura chache sana katika uchaguzi wa 1060 kati ya John F. Kennedy na Richard M. Nixon na uchaguzi wa 1880 kati ya James Garfield na Winfield S. Hancock.
Tofauti za kura za majimbo ni za muhimu sana, lakini kura za wananchi zilionyesha kwa uwazi ni kwa kiasi gani taifa limegawanyika. Taifa limegawanyika kisiasa, lakini yale maswala ya mgawanyiko yameleta pia mgawanyiko katika mataifa yote. Uchaguzi wa mwaka huu (2012) umeweka wazi kwamba Waamerika wamegawanyika juu ya maswali ya msingi. Waamerika wemegawanyika katika kambi zinazoainisha na kuutazama ulimwengu katika mambo kadhaa ya msingi. Ikumbukwe kwamba uchaguzi haukusababisha mgawanyo huu bali umeuibua tu. Mgawanyiko huu katika ngazi ya kimataifa unamfanya Rais Obama kuingiwa na hofu katika kushughulikia changamoto za kisiasa, lakini matatizo na changamoto ni kubwa zaidi ulimwenguni hasa zile za kikanisa/kidini.

Uchaguzi uliobadilika na unaobadilika
Mabadiliko ya kimsingi kwa chaguzi za Amerika yalikuwa dhahiri. Mbadiliko makubwa ya watu namaanisha kuwa uchaguzi uliwa wa kikabila, mila & desturi, na mitazamo iliyotofautiana sana. Uchaguzi umekuwa sio kitu cha kuheshimiwa tena. Tafiti za hivi karibuni zilizofanywa zinaonyesha kuwa kiashirio kimojawapo kikubwa cha upigaji kura ni kiasi cha mahudhurio kanisani/ au kuwa muumini na muhudhuriaji mzuri kanisani. Kwa sasa ni waamerika wachache tu wanaohudhuria makanisani, na utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa 20%  ya Waamerika wote hawana dini yeyote. Hivyo basi kuugeuza uchaguzi kuwa wa kidini zaidi unaweza kuliletea Taifa madhara makubwa na mabaya sana.
Amerika inaendelea kuwa mji, na hili pia limesababisha hali ya upigaji kura. Wapiga kura wapya (vijana) hawajaainishwa kikabila, kwa mtazamo wa muda mrefu chaguzi zinabadilika sana. Waamerika wachache wameoa na ni wachache tu wenye watoto manyumbani kwao. Hili pia, linabadilisha tabia na hali ya upigaji kura. Hizi ni miongoni mwa sababu chache zinazoweza kusababisha mabadiliko ya kimsingi katika Taifa.

Mwisho wa muungano wa warepublican
Ingawaje warepublican wengi wanatiwa moyo kwa kuwa na kura nyingi za uwakilishi, kura za majimbo zitaendelea kukisababishia chama hiki matatizo makubwa sana. Ramani hii haiwaongezei chochote wanarepublicans kwa hali halisi iliopo sasa, bali ni kuibomoa taswira nzima ya chama.  Kwa urahisi niseme hivi, Chama cha Republican hakitaweza kushinda urais kwa sasa mpaka kimebadilika na kuwa ni chama cha vijana wa kiamerika na Wahispanic Amerika. Vinginevyo, kitakuwa ni chama cha kizazi cha wazee waliostaafu wasiopenda mabadiliko. Nafasi ya chama juu wa wahamiaji ni ya hatari sana, na inashangaza hata maadili ya chama chake chenyewe.
Hakuna chama kitakacho shinda kikionekana hakina moyo. Hakuna chama kitashinda kikionekana ni cha weupe na waamerika wazee. Hakuna chama kitashinda kikionekana kinaelekea tulikotoka badala ya kuonyesha njia tunakoenda. Chama cha Republican kisingeweza kushinda kiti cha urais kwa kutumia vigezo vya udhaifu wa uchumi na janga la ukosefu wa ajira, kama mwandishi wa habari George aliweza kusema, chama ambacho hakitashinda kwa mazingira haya ni lazima kitafute namna nyingine ya utendaji kazi.
Chama cha Republican hakinabudi kujitathimini kwa muda wa kutosha na kuiweka sawa taswira na mwelekeo wake. Mchuano huu ni wa muhimu sana, na ni wa maana sana miongoni mwetu tunaothamini na kuhusika sana na mambo kadha wa kadha.

Janga la mmomonyoko wa maadili
Wainjilisti wa Kikristo lazima wautazame uchaguzi huu wa mwaka 2012 katika Taifa hili kubwa la Amerika kama ni janga la kimaadili. Kuchaguliwa kwa Rais Obama unamrudisha Rais anaetetea utoaji mimba katika ikulu ya Marekani (White House), Mapema atakapo pitisha sheria ya kuzikubali ndoa za njinsi moja (same-sex marriage). Rais Obama inawezekana akawa na fursa ya kumteua jaji mmoja au zaidi wa mahakama kuu na kwa uhakika watakubaliana juu ya falsafa ya katiba ya Nchi.
Zaidi ya hapo, majimbo mawili, Maine and Maryland, yalihalalisha ndoa za jinsi moja. Jimbo la Washington pia liko mbioni kuhalalisha mpango huo. Juhudi za kufanya marekebisho ya kuzuia ndoa za jinsi moja ziligonga mwamba katika jimbo la Minnesota. Hii ilikuja mara baada ya majimbo 33 kupitisha ainisho la ndoa kama ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke. Mara baada ya ushindi huu wa majimbo 33, usiku wake majimbo kadhaa yalitangaza kujitoa na hivyo kukubaliana na kuhalalisha ndoa za jinsi moja, majimbo haya ni Maine and Maryland (na labda Washington) yakawa ni majimbo ya kwanza kuhalalisha muunganiko wa ndoa za jinsi moja kwa kupiga kura.
Kwa uwazi kabisa, tunakabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili hapa Amerika, na changamoto kubwa zaidi miongoni mwetu tunaojali na wenye wivu juu ya maswala haya. Tunakabiliana na changamoto ya dunia nzima ambayo ni kubwa zaidi ya changamoto ya kisiasa, ni lazima tujifunze kuwashawishi waamerika katika kushirikishana hukumu za dhamira zetu za kimaadili juu ndoa, jinsi na utakatifu wa maisha na mambo kadhaa ya kimaadili. Hii haiwezi ikawa ni jambo rahisi. Lakini linahitaji mwitikio wa pamoja na haraka katika kulishughulikia.

Sio tu kuhusu siasa
Wakristo hawapaswi kuona vitendo vya kisasa kama ndio mwisho wa mambo, bali tu ni kama mwanzo na njia. Hatuwezi kutafuta wokovu kupitia mabox ya kura pekee, na kamwe tusimtegemee masia wa kisiasa. Wakristo lazima wachukue wajibu wa kisiasa, kusimika upendo wa Mungu na katika kuwapenda majirani. Sisi tunhusika sana na ulimwengu huu, japo ni kwa kiasi Fulani tu. Lengo letu kuu ni Injili ya Yesu Kristo.
Kuishi katika ulimwengu lakini tukiwa sio wa ulimwengu huu haijawahi kuwa rahisi. Uchaguzi huu wa Amerika umeainisha changamoto tunazo kabiliana nazo sasa na wajibu tunaotakiwa kuufuata na kuutenda.
Kwan nchi za ulimwengu wa tatu na zinzoendelea zina kila sababu ya kujifunza kwa yote yanayotokea katika mataifa makubwa kama Amerika. Wakristo pia lazima wawe macho kuhakikisha kwamba mpango wa Mungu unasimama. Tusipoomba Mungu, wanawake waombolezaji wasiposimama na kuliombea taifa. Mambo mabaya kama ndoa za jinsi moja zitafika mpaka huku kwetu na zitaingia mpaka makanisani haya makanisa ya Kipentekoste.Ni wajibu wetu kama watu wa Mungu kuomba Mungu kwa bidii tukipambana na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho.


No comments:

Post a Comment