Mkutano wa wakristo waliopoteza makao yao kufuatia ghasia Nigeria |
Kundi la kiisilamu la Boko Haram
nchini Nigeria, na vikosi vya usalama, wote wametuhumiwa na shirika la
kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International kwa kufanya vitendo vya
kukiuka haki za binadamu hasa katika eneo la Kaskazini lenye waisilamu wengi.
Boko Haram, ambalo jina lake
linamaanisha elimu ya kimagharibi imeharamishwa, kufanya harakati za kuiangusha
serikali na kuunda taifa la kiisilamu.
Siku ya Jumapili, kanisa
lilishambuliwa na kusababisha vifo vya watu wanane mjini Kaduna, mojawapo ya
miji ambayo imeathirika kutokana na mzozo unaoendelea kati ya serikali na Boko
Haram.
Ingawa hawajakiri kufanya
mashambulizi hayo, kundi hilo limewajibika wakati lilipofanya mashambulizi
Kaskazini na kati kati mwa Nigeria.
Obadiah Diji, kiongozi mmoja wa
vijana wa kikristo mjini Kaduna, alisimulia BBC ambavyo maisha yamebadilika
mjini humo.
“ watu wanaogopa hata kutoka nje
usiku au hata kukaa nje tu kunywa pombe au hata kula samaki.
Nimeishi mjini Kaduna karibu maisha
yangu yote na nimejawa na huzuni sana nikiona ambavyo umegawanyika sana kwa
,misingi ya kidini.
Waisilamu wanaishi ambako idadi yao
ni kubwa, wakristo nao vile vile. Kwa hivyo makundi hayo mawili ya watu,
yanaishi maisha yao kivyao bila kutangamana
Sio kawaida kuwa hivi. Wakati mmoja
tulijivunia kwa sababu ya umoja uliokuwa unadhihirika hapa Kaduna na kila mtu
alikuwa anakaribishwa hapa.
Wanigeria wakifanya maombi |
Ingawa kulikuwa na migawanyiko,
wakristo na waisilamu waliishi kwa pamoja. Tulikuwa tunatembeleana . Watoto wetu
walisoma katika shule koja , wakijifunza kutoka kwa kila mmoja kuhusu dini na
tamaduni zao.
Watu hata walioana licha ya dini zao
mfano mamangu wa kambo alibadili dini na kuwa muisilamu na kisha akaoa
muisilamu.
Dadangu pia aliolewa na muisilamu
ingawa alisalia kuwa mkristo.
Kuna ndoa nyingi kama hizo mjini
Kaduna. Haikuwahi kusababisha tatizo lolote. Watu waliheshimiana na
kustahimiliana , sio chuki wala ghasia.
Mambo yalibadilika mwaka 2000 wakati
Kaduna ilishambuliwa kwa mara ya kwanza na mzozo wa kidini ambao unachochewa na
makundi yanayotaka sheria za kiisilamu.
Hapo ndipo makundi yaliyohisi
kutengwa yalijitokeza. Watu walitoroka makwao kwa sababu ya ghasia. Wakristo
walijipata wakiishi katika eneo lao mjini kaduna huku waisilamu nao wakijipata
wakiishi maeneo yao.
Nimekuwa nikipinga maeneo
yaliyotengewa jamii moja na ndio maana bado naishi na mke wake na watoto wetu
wanne katika eneo ambalo ni la waisilamu wengi.
Wanawake katika mikutano kadhaa
maeneo ya Kaskazini wamepigwa marufuku kubeba vibeti kanisani. Makanisa mengi
sasa yana vifaa vya kuwachungua watu wanaoingia kanisani ikiwa wana silaha
yoyote au la.
Wanawake wanazuiwa kubeba vibeti kwa
sababu mshambuliaji anaweza kuingia kanisani akiwahadaa watu kuwa ni muumini
kumbe amebeba silaha kwenye kibeti chake.
Kwa hivyo maisha yetu ya kidini
yameathiriwa sana pamoja na hata maisha ya kijamii.
Sasa tunaishi maisha ya faragha muda
wote tukikaa nyumbani. Ni polisi pekee ambao wanapatikana barabarani usiku.
Lakini ghasia zimewafanya watu kuwa
na imani sana.
Wanapata imani hiyo kutoka kwa
bibilia ambayo inasema tutapitia mateso kama alivyoteswa Yesu .
Ujumbe ambao sisi wakristo
tunasambaza ni kwamba waisilamu ni watu wazuri na ni wachache miongoni mwao
ambao wanasababisha vurugu, hatapaswi kuvuruga uhusiano kati ya jamii hizo
mbili.
Wakati waisilamu waliposherehekea
Eid al-Kabir, tuliungana nao katika barabara moja mjini , tulikula pamoja na
kusherehekea ili kuimarisha makubaliano ya amani na umoja..
Kwa wakati huu, hata mizozo ya
kisiasa inageuka na kuwa ya kidini. Siku mbili baadaye, kanisa lilishambuliwa
kwa mabomu lakini hilo halitasitisha juhudi zetu za kupatana.
Shule za pamoja
Wakristo na wasilamu husoma hapa na
wao ndio tunawategmea kwa mustakabali wetu.
Tunatumai watakuwa na kusoma pamoja
na kufahamu kuwa tunaweza kuwa watu wa dini mbali mbali lakini bado tunaweza
kuishi pamoja.
Washambuliaji wa kujitoa mhanga,
wamekuwa wakilenga makanisa Kaskazini mwa Nigeria. Ili kupunguza vurugu katika
jamii lazima tudurusu mfumo wa siasa zetu.
Tunahitaji kuuliza , je Nigeria
ilikuwa sawa kuanza kutumia mfumo wa demokrasia ya kimagharibi?
Wanawake waliopoteza jamaa zao kwenye shambulizi la Boko Haram |
Hata hatukuwahi kuwa na kiwango hiki
cha ghasia wakati wa utawala wa kijeshi.
Na hii sio kusema eti lazima
tuwakabidhi mamlaka majenerali jeshini.Badala yake, lazima tuangalie,mifumo ya
utawala wa kizamamani kabla ya kuja kwa wakoloni.
Tunaweza kujifunza kutoka kwa mifumo
hii na kubadili namna ambavyo tunatawaliwa ili ufisadi upungue ,viwango vya
umaskini vishuke na kisha ghasia pia ipungue.
Mfumo wa kisasa wa maisha
umesababisha athari kuliko manufaa.
Na leo ni serikali za magharibi
pamoja na makampuni ambayo ni chanzo cha vifo vya watu wetu. Makampuni hayo
ndio yanatengeza silaha na kuuza kwa mataifa yetu ambayo yanazitumia kwa vita
mfano Nigeria na kwingineko.''
No comments:
Post a Comment