Tuesday, November 6, 2012

NEW LIFE BAND KATIKA HUDUMA NCHINI MAREKANI



New Life band kutoka jijini Arusha inazidi kuendelea na ziara yake ya kihuduma huko nchini Marekani, ambapo imekuwa ikifanya matamasha mbalimbali yaliyoandaliwa na marafiki zao walioko nchini humo ambao wanasapoti huduma ya band hiyo kongwe hapa nchini. 

Ambapo kwa mujibu wa mmoja wa waimbaji nyota wa band hiyo kama alivyokaririwa katika page yake ya Facebook amesema wametoka katika mji wa Ventura na kupitia China town Los Angeles kisha Palm Desert ambako wameshiriki katika ibada tatu za katika kanisa la Hope Lutheran Palm Desert, ambapo kwasasa wapo mji wa Long Beach ambako watakaa siku mbili kisha kuelekea mji wa Orange. Zaidi waimbaji hao wameomba watanzania kuendelea kuwaweka katika maombi. Ni takribani miezi mitatu sasa tangu band hiyo iende nchini humo kwa huduma
Peter Abednego katika pozi huko Marekani.


Baadhi ya waimbaji wa New Life band katika picha baada ya ibada jumapili kanisa la Kilutheri la Gloria Dei.


New Life band ndani ya pensi, kitamaduni zaidi ndani ya mji wa Los Angeles Marekani.
    
Baada ya huduma, ni wakati wa kuburudika. Picha kwa hisani ya Peter Abednego Hango.




Polisi nchini Kenya wanasema watu kama 7 wamejeruhiwa kwenye shambulio la guruneti dhidi ya kanisa katika mji wa Garissa.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na televisheni ya Kenya, KTN, wanasema idadi ya watu waliojeruhiwa inaweza kuwa kubwa zaidi na baadhi ya majeruhi ni mahututi.
Afisa mmoja amesema kanisa hilo lilikuwa ndani ya kambi ya polisi na guruneti liling'oa paa wakati wa ibada.
Wengi waliojeruhiwa ni askari polisi.
Mji wa Garissa uko karibu na mpaka wa Somalia.
Mwezi wa Julai watu 15 walikufa katika mashambulio kama hayo dhidi ya makanisa mjini Garissa.
Wakati huo huo
Kanisa la Copt la Misri limemchagua papa mpya atayewaongoza Wakristo wanaokisiwa kuwa milioni-8 nchini Misri.

Askofu Tawadros ambaye amechaguliwa kuwa papa mpya.
Jina la Askofu Tawadros liliteuliwa na mtoto kati ya majina matatu yaliyoandikwa kwenye vikaratasi vilivowekwa kwenye jagi. Papa mpya ni Askofu Tawadros mwenye umri wa miaka 60, na alikuwa msaidizi wa Papa Shenouda wa tatu ambaye alifariki mwezi wa March baada ya kuongoza kanisa hilo kwa miaka 40.
Uteuzi huo ulitokea katika ibada maalumu iliyofanywa katika Kanisa la Saint Mark's mjini Cairo.
Mwandishi wa BBC mjini Misri anasema papa mpya ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na maarifa ya uongozi; na kwamba atahitaji sifa hizo katika nchi ambayo inajadili mchango wa Uislamu baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani Rais Hosni Mubarak.
Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood, kinachoongoza serikali, alinena kuwa wana matumaini kwamba watakuwa na ushirikiano na papa mpya.
Habari kwa mujibu wa BBC.



No comments:

Post a Comment