Thursday, September 27, 2012

KWA NINI MABAYA HUWAPATA WATU WEMA


Hili ni mojawapo la maswali magumu katika uchambuzi wa bibilia. Mungu ni wa milele, hana mwisho, anajua kila kitu, yuko kila mahali na ananguvu kuliko mtu yeyote au kitu chochote. Ni kwa nini wanadamu (hawaishi milele, hawajui mambo yote, hawako kila mahali, hawana nguvu zote) wanatarajia kuelewa njia za Mungu? Kitabu cha Ayubu kinashugulikia hali hii. Mungu alimuruhusu shetani kufanya chochote alichokitaka kwa Ayubu lakini si kumuua. Je Ayubu alifanya nini? “Tazama, ataniua; sina tumaini; Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake” (Ayubu 13:15). “Akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.” (Ayubu 1:21). Ayubu hakuelewa ni kwa nini Mungu alimuruhusu shetani afanye aliyoyafanya, lakini alijua Mungu ni mwema na kwa hivyo aliendelea kumtumainia. Hatimaye hiyo yatupasa tuwe na msimamo kama huo.

Ni kwa nini maovu yanawapata watu wema? Jibu la kibibilia ni, hakuna watu “wema”. Bibilia inaweka wazi kabisa kwamba, wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu(Mhubiri 7:20; Warumi 6:23; 1Yohana 1:8). Warumi 3:8-18 haiweki vizuri kama hakutakuwa na watu wenye “haki” “kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawakuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.” Kila mwanadamu chini ya jua alistahili kutupwa jehanamu. Kila nukta ya dakika tunapokuwa na uhai ni kwa neema na rehema za Mungu. Hata tunapo pitia machungu katika dunia hii, Mungu ni wa huruma tukilinganisha na tunayostahili ambayo ni jehanamu ya milele, ziwa la moto.
MACHOZI YAMEKUWA CHAKULA CHANGU

MUNGU NAOMBA UNISAIDIE


Swali nzuri laweza kuwa “Ni kwa nini Mungu anayaruhusu mazuri kuwatokea waovu?” Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Mbali na uovu, unyonge, na hali ya dhambi ya watu wa ulimwengu huu, Mungu bado atupenda. Anatupenda ya kutosha hadi kufa ili achukue hukumu ya dhambi zetu (Warumi 6:23). Tukimpokea Yesu kama Mwokozi wa maisha yetu (Yohana 3:16; Warumi 10:9), tutasemehewa na tumeaidiwa  mji wa milele mbinguni (Warumi 8:1). Tunachostahili ni jehanamu, na  sasa tumepewa  uzima wa milele kama tutakuja kwa Yesu kwa imani.

Naamu, wakati mwingine mambo maovu huwapata watu wanaonekana hawastahili kuyapata. Lakini Mungu huyaruhusu hayo kutokea kwa kusudio lake, haijalishi kama tunayaelewa. Faida (zaidi) ya hayo, kwa hivyo lazima tukumbuke kuwa Mungu ni mwema, mwenye haki, na ni wa huruma. Kila mara mambo yanapotupata ambayo hatuwezi kuelewa sababu.  Ingawa badala ya kuuona  wema wa Mungu, jukumu letu liwe kumtumainia Mungu. “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako” (Mithali 3:5-6).

Tuesday, September 25, 2012

WAKRISTO WENGI HAWASOMI BIBLIA


Ni ukweli usiopingika kuwa “ Neno la Mungu yaani Biblia ndo kiongozi, uzima na nguvu pekee ya wakristo”.  Cha kushangaza ni kwamba wakristo wengi hawatiliii maanani katika kuisoma Biblia. Utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa Wakristo wengi waendao kanisani hawana tabia ya kulisoma neno la Mungu kila siku.
Utafiti uliofanywa na shirika la utafiti la LifeWay unaonyesha kuwa asilimia tisini  (90%) ya wakristo wanaoenda kanisani wanakubali kwa kutumia sentesi inayosema kuwa, "Ninapenda kumpendeza na kumheshimu YESU katika yote nifanyayo." Lakini asilimia kumi na tisa  (19%) tu ndiyo wanasoma Biblia kila siku, na 25% husoma Biblia siku chache katika juma.
Ed Stetzer, Rais wa shirika la utafiti la LifeWay alisema "Biblia inahusika moja kwa moja katika kuleta matokeo katika kila eneo la ukuaji wa kiroho". Asilimia kumi na nne (14%) ya wakristo wanasema husoma Biblia mara moja kwa Juma," 22% walisema  "husoma mara moja kwa mwezi" au "mara chache katika mwezi," na (18%) husoma mara chache sana au huwa hawasomi kabisa.
Stetzer alisema, “Unaweza kumfuata Kristo na ukaona ukristo kama ni chanzo cha UKWELI”. Lakini kama ukweli huu haupenyi katika mawazo, matarajio na matendo yako, basi haujaungamanishwa na UKWELI. Ukiwa msomaji mzuri wa Biblia, hakika Biblia itakuwa sehemu ya maisha yako, na kamwe hautapotea njia kwani utakuwa na kiongozi shupavu wa kukuongoza.
NENO LA MUNGU LAZIMA LIWE NDO RAFIKI YETU KILA SIKU

SOMA BIBLIA NA FAMILIA YAKO, HASA WAKATI WA IBADA ZA NYUMBANI

SOMA BIBLIA KILA SIKU MAANA NDIYO UZIMA WAKO
  Kila usomapo Biblia hakikisha unafanya mambo yafuatayo: -
  1. Fanya maombi kabla hujaanza kusoma Biblia, mwambie Roho Mtakatifu akusaidie kulielewa neno unalokwenda kulisoma. Kumbuka Roho Mtakatifu ndiyo, mwandishi mkuu wa Biblia hivyo atakufafanulia kila andiko utakalolisoma na utaelea vizuri.
  2. Kila unaposoma Biblia kubali Mungu akufundishe usiwe mbishi.
  3. Usiwe na mtazamo wowote katika akili yako wakati unasoma Biblia, jifanye hujui chochote ili Mungu apate nafasi ya kukufundisha. Watu wengi wamepotea na kukosea kwani wanaposoma Biblia tayari huwa na mtazamo fulani juu ya kitu fulani ambacho huziba nafasi ya kufundishwa na Mungu.
  4. Akili yako iwetayari kufundishwa na Mungu mwenyewe.

Monday, September 3, 2012

KONGAMANO KUBWA LAFANA SINZA REFUGEE CENTER


Ni kongamano kubwa la aina yake lililojaa miujiza na ishara nyingi za Roho mtakatifu lililofanyika katika kanisa la TAG Sinza Refugee Center.Watumishi wa Mungu waliovikwa nguvu za Mungu na madhihirisho ya nguvu za Roho mtakatifu, wakiongozwa na Mch. Seiko sheyo (Mwenyeji) pamoja na Mch. Joseph Marwa (mgeni muhubiri na katibu wa jimbo la zanzibar) walihubiri kwa nguvu za Mungu. Sinza imetetemeshwa kwa nguvu za Mungu, hakika Mungu anawatumia watumishi wake kukionya na kukielekeza kizazi cha leo kimrudie Mungu na kulifundisha kanisa la Mungu kusimama na kuitenda kazi ya Mungu.
Akihubiri kwa nguvu za Roho mtakatifu Mch.Joseph Marwa kutoka Zanzibar alisema, Kizazi cha leo kinahitaji madhihirisho ya nguvu za Mungu na wala si maneno matupu. Tunapoujulisha ulimwengu juu ya nguvu za Mungu wetu lazima nguvu zake  zionekane kuwa ushuhuda kwa watu wote. Akihubiri kutoka kitabu cha cha Waamuzi 2:6-10, kwamba kikainuka kizazi kingine nyuma yao ambacho hakikumjua Mungu..........Alisisitiza kizazi chetu kinahitaji kujulishwa juu ya Mungu wa Mbinguni mwenye nguvu na uwezo wa ajabu. Akifundisha kwa mifano alisema kulipita vizazi vinne kama ifuatavyo;-
(1)         Kizazi cha Musa; Kiliona bahari ikipasuka mbele yao, kilikula kwale jagwani, kilikula mana jangwani iliokuwa ikidondoka kila siku toka mbinguni,kilisikia sauti ya Mungu lakini hakikumwamini Mungu, na Mungu akaadhimia kukiangamiza jangwani badala yake wakapona Yoshua na Kalebu.
(2)         Kizazi cha Yoshua na kalebu; kizazi hiki kilitumia uzoefu wa mababu zao, ingawaje Mungu alitaka kitumie uzoefu mpya kwa kufundishwa na Mungu mwenyewe. Hivyo Mungu alijifunua upya kwa kizazi hiki.
(3)         Kizazi cha wazee: hichi ni kizazi kilichozaliwa jangwani na ambacho kiliingia katika nchi ya ahadi.
(4)         Kikainuka kizazi kipya; Biblia inasema baada ya vizazi vyote vya kwanza kupita kikainuka kizazi kipya kisicho mjua Mungu. Kizazi hiki kilikuwa na matatizo yafuatayo (1) Hakikumjua Mungu (2) Hakikuwahi kuiona ile kazi Mungu alifanya wakati wote walipokuwa Jangwani. Kizazi hiki kinafanana na kizazi cha leo.
Tunahitaji Mungu atendae kazi katika kizazi cha leo, tunahitaji watumishi wa Mungu wenye nguvu za Mungu watende kazi ya Mungu kwa madhihirisho ya Roho mtakatifu kuwa ushuhuda kwa watu wote duniani. Kizazi cha sasa kinahitaji Matendo makuu na miujiza na ishara na wala sio maneno tu.Biblia ina sema “Yesu kristo ni yeye yule jana leo na hata milele”
Rafiki yangu msomaji kama bado hujampa Yesu maisha yako amua leo akuokoe akufanye mtoto wake hakika ya kale yatapita nawe utakuwa kiumbe kipya.Ebu tazama matukio katika picha jinsi kongamano lilivyo kuwa.
Hii ndo madhabahu ya TAG Sinza Refugee Center

Kikundi cha kusifu na kuabudu kikiwa kazini siku ya Kongamano

Kikundi cha kusifu na kuabudu kama kawa

Kiongozi wa kusifu na kuabudu akiwaongoza watu katika kumsifu Mungu

Mwinjilisti Christopher akiwa kikazi zaidi madhabahuni pa Bwana Yesu

Christopher akiwa kazini na kikundi cha kusifu na kuabudu

Mch.Sote (booster) akiwa amejaa nguvu za Mungu tayari kwa kazi

Umati wa watu wakiwa ktk Ibada ya kusifu

Watu wakiserebuka wakati wa kipindi cha kusifu

Haya sasa hapo bariki amen, bariki amen!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kama kawa, watu wote bariki Amen!!!!!!bariki Amen!!!!!

Mwinjilisti Christopher akiwa kazini zaidi

Mch. seiko (mwenyeji) na mch. sote wakiimba yekelekele aaah! zambe wa moyo

Kwaya ya wenyeji wakiimba wakati wa kongamano

Kwaya ya Kijitonyama Anointed wakiimba wakati wa kongamano

Watu wakisikiliza kwa makini wakati K

Kwaya ya Revival magomeni wakiimba wakati wa kongamano

Kijana amani wa kwaya ya Revival magomeni akiwa kazini

Kikombe cha babu akiimba wakati wa kongamano akisaidiana na christopher

Christopher akiimba wimbo wa "saa imefika ya kubarikiwa"

Watu wakibarikiwa na wimbo wa Saa imefika ya kubarikiwa

Watu wakiserebuka wakati christopher akiimba



Mch. Joseph Marwa akihubiri kwa nguvu za Mungu wakati wa kongamano

Mch. Marwa akifundisha kwa mifano aina 4 za vizazi

Ilikuwa ni kazi kwelikweli

Mch. marwa akiwa tayari kufanya maombezi kwa watu wenye shida mbalimbali

Maombezi yakifanyika katika jina la YESU KRISTO

Jopo la watumishi wa Mungu wakifanya maombezi kwa watu wenye shida katika jina la YESU

Tumepewa jina moja la YESU! katika jina la YESU uwe mzima!

Yesu akiwa kazini kwa madhihirisho ya Roho mtakatifu



Funguka katika jina la YESU!

Pokeeni nguvu za Mungu

Watu wakijimimina katika uwepo wa Mungu


Mwinjilisti Christopher akiwa kwenye mitambo

Mama uwe mzima katika Jina la YESU

Funguka katika jina la YESU