Tuesday, September 25, 2012

WAKRISTO WENGI HAWASOMI BIBLIA


Ni ukweli usiopingika kuwa “ Neno la Mungu yaani Biblia ndo kiongozi, uzima na nguvu pekee ya wakristo”.  Cha kushangaza ni kwamba wakristo wengi hawatiliii maanani katika kuisoma Biblia. Utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa Wakristo wengi waendao kanisani hawana tabia ya kulisoma neno la Mungu kila siku.
Utafiti uliofanywa na shirika la utafiti la LifeWay unaonyesha kuwa asilimia tisini  (90%) ya wakristo wanaoenda kanisani wanakubali kwa kutumia sentesi inayosema kuwa, "Ninapenda kumpendeza na kumheshimu YESU katika yote nifanyayo." Lakini asilimia kumi na tisa  (19%) tu ndiyo wanasoma Biblia kila siku, na 25% husoma Biblia siku chache katika juma.
Ed Stetzer, Rais wa shirika la utafiti la LifeWay alisema "Biblia inahusika moja kwa moja katika kuleta matokeo katika kila eneo la ukuaji wa kiroho". Asilimia kumi na nne (14%) ya wakristo wanasema husoma Biblia mara moja kwa Juma," 22% walisema  "husoma mara moja kwa mwezi" au "mara chache katika mwezi," na (18%) husoma mara chache sana au huwa hawasomi kabisa.
Stetzer alisema, “Unaweza kumfuata Kristo na ukaona ukristo kama ni chanzo cha UKWELI”. Lakini kama ukweli huu haupenyi katika mawazo, matarajio na matendo yako, basi haujaungamanishwa na UKWELI. Ukiwa msomaji mzuri wa Biblia, hakika Biblia itakuwa sehemu ya maisha yako, na kamwe hautapotea njia kwani utakuwa na kiongozi shupavu wa kukuongoza.
NENO LA MUNGU LAZIMA LIWE NDO RAFIKI YETU KILA SIKU

SOMA BIBLIA NA FAMILIA YAKO, HASA WAKATI WA IBADA ZA NYUMBANI

SOMA BIBLIA KILA SIKU MAANA NDIYO UZIMA WAKO
  Kila usomapo Biblia hakikisha unafanya mambo yafuatayo: -
  1. Fanya maombi kabla hujaanza kusoma Biblia, mwambie Roho Mtakatifu akusaidie kulielewa neno unalokwenda kulisoma. Kumbuka Roho Mtakatifu ndiyo, mwandishi mkuu wa Biblia hivyo atakufafanulia kila andiko utakalolisoma na utaelea vizuri.
  2. Kila unaposoma Biblia kubali Mungu akufundishe usiwe mbishi.
  3. Usiwe na mtazamo wowote katika akili yako wakati unasoma Biblia, jifanye hujui chochote ili Mungu apate nafasi ya kukufundisha. Watu wengi wamepotea na kukosea kwani wanaposoma Biblia tayari huwa na mtazamo fulani juu ya kitu fulani ambacho huziba nafasi ya kufundishwa na Mungu.
  4. Akili yako iwetayari kufundishwa na Mungu mwenyewe.

1 comment: