Ni kongamano
kubwa la aina yake lililojaa miujiza na ishara nyingi za Roho mtakatifu
lililofanyika katika kanisa la TAG Sinza Refugee Center.Watumishi wa Mungu
waliovikwa nguvu za Mungu na madhihirisho ya nguvu za Roho mtakatifu,
wakiongozwa na Mch. Seiko sheyo (Mwenyeji) pamoja na Mch. Joseph Marwa (mgeni muhubiri
na katibu wa jimbo la zanzibar) walihubiri kwa nguvu za Mungu. Sinza
imetetemeshwa kwa nguvu za Mungu, hakika Mungu anawatumia watumishi wake
kukionya na kukielekeza kizazi cha leo kimrudie Mungu na kulifundisha kanisa la
Mungu kusimama na kuitenda kazi ya Mungu.
Akihubiri kwa
nguvu za Roho mtakatifu Mch.Joseph Marwa kutoka Zanzibar alisema, Kizazi cha
leo kinahitaji madhihirisho ya nguvu za Mungu na wala si maneno matupu.
Tunapoujulisha ulimwengu juu ya nguvu za Mungu wetu lazima nguvu zake zionekane kuwa ushuhuda kwa watu wote.
Akihubiri kutoka kitabu cha cha Waamuzi 2:6-10, kwamba kikainuka kizazi kingine
nyuma yao ambacho hakikumjua Mungu..........Alisisitiza kizazi chetu kinahitaji
kujulishwa juu ya Mungu wa Mbinguni mwenye nguvu na uwezo wa ajabu. Akifundisha
kwa mifano alisema kulipita vizazi vinne kama ifuatavyo;-
(1)
Kizazi cha Musa; Kiliona bahari
ikipasuka mbele yao, kilikula kwale jagwani, kilikula mana jangwani iliokuwa
ikidondoka kila siku toka mbinguni,kilisikia sauti ya Mungu lakini hakikumwamini
Mungu, na Mungu akaadhimia kukiangamiza jangwani badala yake wakapona Yoshua na
Kalebu.
(2)
Kizazi cha Yoshua na kalebu;
kizazi hiki kilitumia uzoefu wa mababu zao, ingawaje Mungu alitaka kitumie
uzoefu mpya kwa kufundishwa na Mungu mwenyewe. Hivyo Mungu alijifunua upya kwa
kizazi hiki.
(3)
Kizazi cha wazee: hichi ni kizazi
kilichozaliwa jangwani na ambacho kiliingia katika nchi ya ahadi.
(4)
Kikainuka kizazi kipya; Biblia
inasema baada ya vizazi vyote vya kwanza kupita kikainuka kizazi kipya kisicho
mjua Mungu. Kizazi hiki kilikuwa na matatizo yafuatayo (1) Hakikumjua Mungu (2)
Hakikuwahi kuiona ile kazi Mungu alifanya wakati wote walipokuwa Jangwani.
Kizazi hiki kinafanana na kizazi cha leo.
Tunahitaji
Mungu atendae kazi katika kizazi cha leo, tunahitaji watumishi wa Mungu wenye
nguvu za Mungu watende kazi ya Mungu kwa madhihirisho ya Roho mtakatifu kuwa
ushuhuda kwa watu wote duniani. Kizazi cha sasa kinahitaji Matendo makuu na
miujiza na ishara na wala sio maneno tu.Biblia ina sema “Yesu kristo ni yeye yule
jana leo na hata milele”
Rafiki yangu
msomaji kama bado hujampa Yesu maisha yako amua leo akuokoe akufanye mtoto wake
hakika ya kale yatapita nawe utakuwa kiumbe kipya.Ebu tazama matukio katika
picha jinsi kongamano lilivyo kuwa.
|
Hii ndo madhabahu ya TAG Sinza Refugee Center |
|
Kikundi cha kusifu na kuabudu kikiwa kazini siku ya Kongamano |
|
Kikundi cha kusifu na kuabudu kama kawa |
|
Kiongozi wa kusifu na kuabudu akiwaongoza watu katika kumsifu Mungu |
|
Mwinjilisti Christopher akiwa kikazi zaidi madhabahuni pa Bwana Yesu |
|
Christopher akiwa kazini na kikundi cha kusifu na kuabudu |
|
Mch.Sote (booster) akiwa amejaa nguvu za Mungu tayari kwa kazi |
|
Umati wa watu wakiwa ktk Ibada ya kusifu |
|
Watu wakiserebuka wakati wa kipindi cha kusifu |
|
Haya sasa hapo bariki amen, bariki amen!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! |
|
Kama kawa, watu wote bariki Amen!!!!!!bariki Amen!!!!! |
|
Mwinjilisti Christopher akiwa kazini zaidi |
|
Mch. seiko (mwenyeji) na mch. sote wakiimba yekelekele aaah! zambe wa moyo |
|
Kwaya ya wenyeji wakiimba wakati wa kongamano |
|
Kwaya ya Kijitonyama Anointed wakiimba wakati wa kongamano |
|
Watu wakisikiliza kwa makini wakati K |
|
Kwaya ya Revival magomeni wakiimba wakati wa kongamano |
|
Kijana amani wa kwaya ya Revival magomeni akiwa kazini |
|
Kikombe cha babu akiimba wakati wa kongamano akisaidiana na christopher |
|
Christopher akiimba wimbo wa "saa imefika ya kubarikiwa" |
|
Watu wakibarikiwa na wimbo wa Saa imefika ya kubarikiwa |
|
Watu wakiserebuka wakati christopher akiimba |
|
Mch. Joseph Marwa akihubiri kwa nguvu za Mungu wakati wa kongamano |
|
Mch. Marwa akifundisha kwa mifano aina 4 za vizazi |
|
Ilikuwa ni kazi kwelikweli |
|
Mch. marwa akiwa tayari kufanya maombezi kwa watu wenye shida mbalimbali |
|
Maombezi yakifanyika katika jina la YESU KRISTO |
|
Jopo la watumishi wa Mungu wakifanya maombezi kwa watu wenye shida katika jina la YESU |
|
Tumepewa jina moja la YESU! katika jina la YESU uwe mzima! |
|
Yesu akiwa kazini kwa madhihirisho ya Roho mtakatifu |
|
Funguka katika jina la YESU! |
|
Pokeeni nguvu za Mungu |
|
Watu wakijimimina katika uwepo wa Mungu |
|
Mwinjilisti Christopher akiwa kwenye mitambo |
|
Mama uwe mzima katika Jina la YESU |
|
Funguka katika jina la YESU |
Mungu wetu ni mwema sana, ibada hii ilikuwa ya kupendeza kwa maana ya kuinua vijana katika kuelekea kuifanya kazi ya Bwana ikiambatana na miujiza mingi.
ReplyDeleteNaona watu wlijaa Roho kwa WIngi sana Mungu ni mwema.
Mh na wakumbuka hawa watumishi walipakwa mafua ya kumsifu Bwana na kuhubiri kwa njia ya uimbaji.
ReplyDeleteMr. Christopher na Ernesty a.k.a Kikombe cha babu.
ujumbe ulionigusa ni kuwa vijana leo tunahitaji kuwa na nguvu za Mungu ili Ulimwengu uone kazi za Yesu na wapate kumwamini Mungu. kazi ni kwa vijana kumtafuta Mungu kutenga Muda wa kusoma Neno la MUNGU ilikujua yale ambayo Mungu alitenda, Macho yetu yAtiwe nuru kumwona Mungu kwa namna ya uungu wake KIUTENDAJI ZAIDI.
ReplyDeletei REMEBER Pastor Marwa.
ReplyDelete