Monday, August 27, 2012

WASAIDIZI WALIOANDALIWA KUKUSAIDIA UFIKIE HATMA YAKO


Leo ni siku ya pili ya semina, ambapo mtume Israel akiwa na ujumbe maalumu kwa ajili ya Tanzania na kanisa la Tanzania.
Alisisitiza, ili mtu afikie na afanye kile kitu Mungu amempangia katika maisha ni lazima wawepo watu wa kumsaidia.Kwa ufupi ni kwamba kuna mtu ana muujiza wako, na siku mtakapo kutana utapata muujiza wako. Hii ina maana kwamba ili wewe ujue na kutimiza lengo la kwa nini upo duniani ni lazima wawepo watu watakao kusaidia kufikia lengo lako. Kwa bahati mbaya watu wengi hawajui kwamba wanatembea na miujiza ya watu wengine hivyohivyo watu wengi hawajui ni nani mwenye muujiza wake/wao. Kitendawili hiki utakitegua kwa maombi tu. Ni maombi yangu leo Mungu akukutanishe na mtu mwenye muujiza wako.
Akihubiri katika ibada ya jumatatu jioni, mtume Israel akiwa na ujumbe usemao “Msaidizi wa kukusaidia ufikie hatma yako” alisoma katika biblia kitabu cha Yohana 2:2 inayohusu Yesu katika harusi ya kana. Ukiwa ni muujiza wake wa kwanza, aliufanya kwa sababu mama yake ni kama alimlazimisha. Baada ya harusi ile kutindikiwa divai, mama yake Yesu (mariamu) alimwambia Yesu kwamba Divai imeisha, Yesu alimjibu mama yake “nina nini na wewe mwanamke? Tukiangalia hapa hili jibu lilionyesha Yesu hakupenda kufanya muujiza kwa sababu muda wake ulikuwa haujafika. Cha muhimu hapa ni kwamba mwisho wa siku Yesu alifanya muujiza wa kugeuza maji kuwa divai safi na njema. Hapa tunaona mariamu aligundua kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kufanya muujiza. Hivyo alimsaidia Yesu kuanza kufanya miujiza. Sisi leo tunahitaji watu kama mariamu watakao weza kutusaidia kugundua kile kitu tunatakiwa kufanya katika maisha yetu. Ndugu yangu unahitaji mtu akusaidie ufikie leongo lako.
Akihubiri huku mahubiri yakiambatana na maombi alisema kwa kutumia mifano mingi kutoka katika Biblia, Mungu alimwambia Musa atafute watu 70 kwa ajili ya kumsaidia afikie lengo katika maisha kupitia huduma aliyokuwa anaifanya. Esta alimuhitaji Mordekai ili afike ikulu Esta 5:6-8. Wakati wana wa Israeli wakiwa vitani Musa alihitaji watu wa kumsaidia kuitegemeza mikono yake ili israeli ishinde vita, hivyo Haruni na Huri wakaitemeza mikono ya Musa na ushindi wakaupata.
Ndugu yangu msomaji najua unatamani sana kufikia lengo katika maisha yako. Ili haya yatimie unahitaji Mungu akuunganishe na watu wenye miujiza yako, na watakao kusaidia ufikie lengo. Ebu tenga muda wa maombi ili Mungu akuongoze kukutana na watu hao. Mungu akubariki sana sana. 
Mtume Eric Israeli akisikiliza ushuhuda wa mama aliyeponywa na uvimbe tumboni

Watu wengi wakiwa wamejiandaa kutoa ushuhuda wa mambo makubwa Mungu amefanya

Kwaya ya Kijitonyama Anointed wakiimba kanisani

Hapa kila mtu alikuwa anapokea toka kwa Mungu wakati wa maombezi

Mtume Israeli na Mch.Dr. Mbwilo wakiombea watu wenye shida Mbalimbali wakati wa semina


Ibada hii ya leo iliambatana na huduma ya kinabii ambapo watu wengi walibarikiwa sana tena sana.
 
Mpenzi msomaji wangu usikose ibada kama hii kesho,Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele.

No comments:

Post a Comment