Sunday, August 19, 2012

MKUTANO WA CA'S SURVEY WAFANA

                                       
Ilikuwa ni siku tatu (17-19/8/2012) za miujiza, matendo na kuvuna roho za watu kutoka katika ufalme wa giza na kuwaingiza katika ufalme wa Mungu.Wapendwa wangu tunaishi katika siku za mwisho ambapo ishara moja wapo ya siku za mwisho ni kwamba Injili itahubiriwa ili kila mtu asikie.

Akihubiri katika viwanja vya kanisa la TAG survey, mwinjilisti Shirima akiongea kwa madaha na kufafanua kwa makini kupitia mafunuo na uwezo wa Roho mtakatifu alilinena neno la Mungu kwa ujasiri.
Wakiwahuburia umati mkubwa uliokuja kusikiliza neno la Mungu, alisoma katika Biblia kitabu cha mathayo 1:18-23 alisema. Yesu ni Mungu pamoja na wanadamu, hata kama wewe utakataa lakini kwetu ataendelea kuwa Mungu.Mstari wa 23 unasema; tazama bikira atachukua mimba naye atamzaa mwana wa kiume naye ataitwa Imanueli maana yake ni Mungu pamoja nasi.

Alifafunua kitaalamu na kutoa maana ya jina Yesu=maana yake ni  "atawaokoa watu na dhambi zao" alisisitiza kwa umakini na kusema. Hakuna ugonjwa unaosumbua dunia na watu wake na ambao hauna dawa kama dhambi. Dhambi haina dawa, kama unakataa kamuulize kiongozi wako wa dini kama atakupa jibu. Leo Mungu amenituma kwenu na katika dunia hii kuwatangazia dawa ya dhambi. Dawa ya dhambi ni YESU. Biblia inasema maana atawaokoa watu wake na dhambi zao. Yesu ndo dawa ya dhambi, ukimpokea leo utapona kabisa. Akihubiri kwa kutoa ushuhuda wake alisema, kabla sijaokoka nilikuwa naumwa, tena mtumwa wa dhambi, dhambi iliharibu maisha yangu kiasi kwamba nilikuwa ni maiti inayotembea. Lakini ashukuriwe YESU kwa kuniokoa na leo naonekana ni mtu kati ya watu.

YESU yupo leo akuokoe, damu yake iliyomwagika msalabani ipo hai leo ikutakase maovu yako. Biblia inasema Ukishaa mpokea yesu leo. Tazama ya kale yatapita nawe utakuwa kiumbe kipya. Nakushauri uamue kumpokea YESU awe Bwana na Mwokozi wako. ebu ungana nami katika kuangalia matukia haya ya mkutano katika picha. Mungu akubariki sana.



 KWAYA YA UBUNGO TAG IKIWA KAZINI MKUTANONI


 KWAYA YA VISION IKIWA KIKAZI ZAIDI


KIJITONYAMA ANOINTED SINGERS (TAG K/NYAMA) IKIWA KAZINI


HAPA NI KAZI TU


VIJANA WA YESU WALIOAMUA KUMTUMIKIA MUNGU


WANA WA IBRAHIMU WAKIWA KIKAZI ZAIDI


WATUMISHI WA MUNGU WAKIWA WANASUBIRI


MCHUNGAJI CHAYO WA TAG SURVEY AKIJIANDAA KUMKARIBISHA MUHUBIRI


MWINJILIST NICODEMUS SHIRIMA AKIHUBIRI INJILI YA YESU KRISTO


WATU WAKITUMIA MUDA WAO VIZURI KWA KUSIKILIZA NENO LA MUNGU


2 comments:

  1. Ayayayayaya.... It was so good, Inapendeza sana kuzinena habari za Yesu kumkomboa mwanadamu, hizi ni habari za uzima. Survey Kwa Yesu.
    Wainjilisti mpo Nena bila Kuchoka.

    Siku hii nakumbuka waliokoka watu watu, tunawaombea waendelee kukua na kuongezeka kiroho.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana Emmanuel kutembelea blog hii, Mungu wangu wa mbinguni akubariki sana sana

      Delete