Maneno haya yalisemwa na mchungaji Anthony kutoka kanisa la TAG Njiro
Arusha alipokuwa akihubiri katika la TAG Kijitonyama, Dar es
Salaam.Alisema kwa msisitizo ujumbe wake ukiambatana na ushuhuda wake
binafsi alisema, Hakika nimemwona Mungu Katika Maisha yangu, hivyo
ninazungumza kitu cha kweli na uhakika. Yesu alisema Mkiwa na Imani
ndogo kama punje ya haradani mtauambia mlima huu ng'oka ukatupwe
baharini. Inasikitisha sana siku za leo tumekuwa na watu wenye uhaba wa
Imani thabiti kwa Mungu aliye hai, badala yake watu wametegemea zaidi
vitu vya Dunia hii vinavyopita na kuharibika.
Watu wa leo (wakristo wa leo) wanashindwa kujitoa asilimia mia moja kwa
Mungu, badala yake wametegemea zaidi kazi zao, vyeo vyao, mali zao,
wazazi wao,utajiri wao badala ya kumtegemea Mungu kwa asilimia mia
moja.Akitoa ushuhuda wake alisema, tulipokuwa Dhambini tulijitoa sana
kwa shetani wengine tulikuwa tunashinda na kukesha vilabuni tukinywa na
kulewa, wengine tulitegemea zaidi kazi zetu. Lakini tulipofukuzwa kazi
tulikosa pa kukimbilia kwa sababu kazi ndo ilikuwa kila kitiu katika
maisha yetu, Vitu vyote vinapita yaani pesa, kazi vyeo na vitu vyote
katika dunia hii, Lakini heri mtu yule amtegemeaye Mungu anbaye Imani
yake iko kwake.
Nikiwa mchungaji nikichunga kanisa moja hapa Tanzania, ilifika wakati
kanisa nililokuwa nikiliongoza wakaniambia kwamba kuanzia leo tutakuwa
hatukupi posho. Nilijipa moyo ilihali nikifahamu kuwa nina kazi
nyingine nafanya, kwani nilikuwa nafanya katika ofisi ya Umisheni katika
kanisa letu la TAG hivyo mahitaji yangu binafsi na familia bado
ningeendelea kuyapata. Ilipofika mwaka 2007 kwa sababu ambazo sizijui
huko nako nikasimamishwa. Mpendwa wangu niliumia sana kwani tumaini
langu sasa lilikwisha. Hapo ndipo nilipoanza kujifunza kumwamini na
kumtegemea Mungu. Wakati namwomba Mungu afanye njia, ndipo neneo
likanitoka "WEWE MUNGU NI AKIBA YANGU" hili neno limekuwa ufungua katika
maisha yangu. Toka wakati ule Mungu amenifungulia milango na baraka za
Mungu sasa zinamiminika kama mvua maishani mwangu. Mimi kwa sasa
siombiombi kwani Mungu amenibariki.Nikutie moyo mkristo mwenzangu hebu
tumwamini MUNGU kwa asilimia moa moja, hakika atafanya katika maisha
yetu.
Ibada hii kubwa iliambatana na kanisa zima kumpongeza mchungaji kiongozi
Dr. Ezekiel Mbwilo ambaye amechanguliwa hivi karibuni kuwa makamu
mwangalizi wa section ya Kinondoni. Hebu fuatana nami kwa kuangalia
matukio katika picha. Mungu akubariki sana msomaji wangu.
No comments:
Post a Comment