Sunday, August 26, 2012

TAMBUA HATMA YAKO YA KIUNGU


Ni swali kubwa linalosumbua na kutesa watu wengi sana. Si ajabu kuona na kusikia kwamba watu wengi duniani hawajui kwa nini wapo?, kwa nini walizaliwa? na kwa nini Mungu aliwaumba?. Wengi wanajiuliza kwa nini wanaishi? Lengo la kuishi ni lipi? Hili limekuwa ni fumbo kwa watu wengi. Inasikitisha sana kwani watu wengi wamekufa pasipokufumbua fumbo hili, wengi bado wanahangaika na wengine wamekata tamaa na kuhalalisha mfumo wa maisha wanayoishi wakisema huu ndio mpango wa Mungu. Ebu ungana nami katika somo hili.
Mtume E.Israeli (kulia) na Mch.Dr.Mbwilo (kushoto)

Mtume Eric Okere Israel akihubiri katika ibada ya jumapili asubuhi na ambayo ilikuwa ni siku yake ya kwanza ya kuanza semina kubwa ya uamsho katika kanisa la TAG Kijitonyama, akiwa na ujumbe usemao “TAMBUA HATMA YAKO YA KIUNGU” (Identifying your divine destiny).Alisema kila mtu duniani alizaliwa,aliumbwa ili atimize mambo au jambo fulani katika maisha yake. Akianza ujumbe wake akisoma katika kitabu cha Warumi 8:28-31 alisema, kabla wewe hujazaliwa Mungu alikujua,na kwa makusudi yake amekupangia hatma yako. Tayari aliandika katika kitabu cha kumbukumbu zake juu ya yale utakayotakiwa kuyatimiza katika maisha yako.
Yeremia 1:4-8 tunaona Mungu anamwambia Yeremia akiwa ni mtoto mdogo yasadikiwa kati ya miaka 5 hadi 7 kwamba kabla hujatungwa mimba nalikujua,kabla hujazaliwa nalikuweka kuwa nabii wa mataifa. Mungu alijua vile Yeremia atakavyokuwa hata kabla hajazaliwa. Aliongeza, Mfalme koreshi alitabiriwa kuzaliwa kwake na kazi ya kujenga hekalu atakayoifanya miaka zaidi ya miaka 300 kabla ya kuzaliwa kwake. Hii inaonyesha kwamba hakuna mtu aliyezaliwa duniani kwa bahati mbaya, kila mtu ana jambo la kufanya katika maisha. Inashangaza kwa nini watu wengi hawajui hatma zao katika maisha? Zifuatazo ni sababu zitakazokusaidia kutambua wewe ni nani na nini hatma yako katika maisha.
1.   Ufunuo wa KIMUNGU: ni muhimu sana kumwomba MUNGU ili afungue macho yako/yetu ili uweze kujua wewe ni nani na nini kusudi la Mungu wewe kuwepo duniani kwa maana ya nini unatakiwa kufanya katika maisha yako. Alitoa mfano akisema, mimi niliota ndoto ya kuwa Muhubiri nikiwa na miaka 10 tu. Ndoto hizi zimekuwa halisi kwangu nikiwa mkubwa hivi leo. Yusufu alitambua hatma yake akiwa na miaka 17. Sisi leo tunahitaji Mungu afungue macho yetu kutambua mambo haya makubwa katika maisha yetu.
2.   Mpangilio/mpango wa KIMUNGU: 1samweli 9:1-3 Mungu aliandaa mpangilio wa sauli kuwa mfalme. Mungu aweza kukutengenezea mazingira ya kufikia hatma yako. Jifunze kile Mungu alifanya kwa sauli.
3.   Uvuvio wa KIMUNGU: Unaweza usione maono, ndoto lakini MUNGU akakuongoza kwa uvuvio wake ndani yako na hatimaye ukagundua nini cha kufanya katika maisha yako.
4.   Utafiti: Watu wengi wamegundua hatma yao kwa kusoma Biblia na vitabu vingine vyenye maarifa na vinavyoongeza marifa ya nini cha kufanya. 2Wafalme 22:3-11, baada ya maneno ya Mungu kusomwa mbele yake akagundua nini hatma yake na nini lengo la Mungu la kumfanya kuwa mfalme.
5.   Tangazo la KIMUNGU:Mungu aweza kusema na wewe kwa sauti ya kusikika juu ya nini watakiwa kufanya na kutimiza katika maisha yako. Mungu alisema na Yeremia kwa sauti kwamba amemuweka kuwa nabii wa mataifa.
6.   Muunganiko wa KIMUNGU: yawezekana ikawa vigumu sana wewe peke yako kujua hasa nini hatma yako au jambo gani unatakiwa kufanya katika maisha yako. Ni vizuri kuambatana, au kukaa na watu waliogundua nini cha kufanya katika maisha. Mungu aweza kuku unganisha  na watu wenye hatma zao tayari, ili kupitia hao nawe uweze kujua nini cha kufanya. Yoshua aliunganishwa na Musa hatimaye akawa kiongozi mkubwa kama Musa.
7.   Ufunuo wa kinabii: Mungu aweza kumleta nabii kukueleza nini hatma yako. Kitabu cha Hosea kinasema kwa unabii taifa linapona na haliangamii. Mungu alimtuma Samweli kumtia mafuta Daudi kuwa mfalme.
Ndugu yangu, ni maombi yangu kwa MUNGU akusaidie kugundua hatma na nini cha kufanya katika maisha yako. Wakati mwingine hautoki kimaisha kwa sababu hujajua wewe unatakiwa uwe nani hasa katika dunia hii. Mungu akubariki sana.  
Kwaya ya Kijitonyama Glory Singers wakiimba ibadani

Kwaya ya Kijitonyama Anointed Singers wakiimba kanisani

Watu wakisikiliza kwa makini ujumbe

Mtume akifundisha kwa mfano

Kama kawaida Yesu ni mtamu sana acha nijimimine kwake

Watu wakijimimina mbele za Mungu wao

3 comments:

  1. The Goodnes of being tought b God. Isay 48:-17

    ReplyDelete
  2. Ni kwei na hakika kuwa watu wengi wanatafuta kujua kwanini Mungu aliwaumba na wengine hawatafakari kabisa ila wanaishi kwa kufanya lolte linalo wapendeza.Ukwelini kwamba wali ili weniwanaojiuliza hwapati jibu, la tu maombi na kufanya kile unachoona ROho Makatifu akielekeza ndio mlango wako wa kujua ni kwanini uliumbwa,
    Neno lilikuwa ni jema sana, ni mambi angu woe watakao fika kwenye semina hii wapokee sawasawa na Mapenzi ya Mungu and to day is day of Profecy, make shure you dont mis.

    ReplyDelete
  3. uwepo ulikuwa mkubwa kaka, watu wameza kwa Roho wa BWANA ANASEMA NA KILA MMOJA WAO, UTKUFU UMRUDIE MWENYEZI.

    ReplyDelete