Friday, November 16, 2012

Jinsi Ibilisi Anavyozuia Maombi Yako






Ndugu msomaji wa blog hii, kati ya makala au masomo ambayo nimeyaandika humu, hili ni somo na ushuhuda mmojawapo wenye nguvu sana ambao, kila mwana wa Mungu atakayeusoma, atapata msukumo wa rohoni usio wa kawaida. Haya ni mafunuo yenye nguvu mno ambayo, hakika yatakuinua kwa kiwango cha juu sana nawe utamshukuru Mungu. Nilipouona ushuhuda huu kwenye mtandao, moyo wangu ulianza kuwaka niweze kuutafsiri harakaharaka na kuuweka kwenye blog hii ili yamkini uweze kuwafikia wapendwa wengi iwezekanavyo.
Huu ni ushuhuda ulioandikwa na Mchungaji John Mulinde wa Uganda kutokana na kile alichosikia kutoka kwa mhusika mwenyewe. Mhusika huyo, mchungaji hajamtaja, lakini alikuwa ni kijana ambaye alimtumikia shetani tangu angali tumboni mwa mama yake. Baadaye, kwa neema ya Bwana kijana huyo aliokolewa, ndipo akaanza kueleza siri hizi za ufalme wa giza na ufalme wa nuru.
Mamilioni ya Wakristo duaniani tunamwomba Mungu wetu kwa ajili ya mahitaji mbalimbali tuliyonayo. Lakini liko swali moja kubwa linalojirudiarudia ndani ya mioyo yetu karibu kila siku. Tunajiuliza, “Nimeomba sana na kwa muda mrefu. Mbona Mungu hajibu…?” Tunabaki bila majibu, tunavunjika moyo, na tunaanza kudhani labda sisi ni wenye dhambi sana ndio maana hatujibiwi.
Ukiifahamu siri iliyomo kwenye ushuhuda huu, utatiwa nguvu sana za rohoni; maana maarifa ndiyo yanayotufanya tuwe na nguvu za Mungu. Tunaenenda kiimani kwa kadiri ya kiwango cha maarifa au ufahamu uliomo ndani yetu. Tukijua sana, tunaweza sana; tukijua kidogo, tunaweza kidogo.
Karibu ujipatie maarifa ambayo Bwana wetu ameruhusu yatufikie. Nami na hakika utamfurahia Bwana kwa kukupigisha hatua nyingine ya imani. Utafanya vema kama ukiweza kuwapatia na wengine somo hili la muhimu sana kwa ajili ya mwili wa Kristo.

Yafuatayo ni maelezo ya Mchungaji John Mulinde:
Napenda nikushirikishe ushuhuda wa kijana mmoja ambaye aliokoka; kijana ambaye alikuwa akimtumikia ibilisi. Na mtu yule alipotoa ushuhuda wake, ulinitia changamoto kubwa sana. Sikutaka kuamini. Ilinibidi nifunge kwa muda wa siku kumi mbele za Bwana, huku nikimuuliza, “Bwana, hivi mambo haya ni kweli?” Na ilikuwa ni katika wakati huo ndipo Bwana alipoanza kunifundisha kile kinachotokea kwenye ulimwengu wa roho pale tunapoomba.
Kijana huyu alizaliwa baada ya wazazi wake kuwa wamejiweka wakfu wao wenyewe kwa lusifa. Wakati bado akiwa tumboni, walifanya matambiko mengi na kumweka wakfu awe mtumishi wa lusifa. Alipozaliwa na kufikisha miaka minne, tayari alianza kutumia nguvu zake za kiroho. Hata wazazi wake walianza kumwogopa! Akiwa na miaka sita, baba yake alimkabidhi kwa wachawi ili akapatiwe mafunzo. Na akiwa na miaka kumi, alikuwa akifanya mambo makubwa katika ufalme wa ibilisi. Alikuwa akiogopwa hata na wachawi wa kawaida.
Alikuwa bado ni kijana mdogo, lakini mambo aliyokuwa anafanya yalikuwa ni mabaya mno. Alikua hadi kufikia miaka ya ishirini akiwa na damu nyingi ya watu mikononi mwake. Aliua watu kila alipotaka. Alikuwa na uwezo wa kutoka nje ya mwili wake kupitia taamuli ya kinjozi (transcendental meditation), yaani kitendo cha kutuliza mawazo na mwili kama wafanyayo Wahindu katika yoga. Tazama mfano HAPA. Katika huko kutaamuli, angeweza hata kunyanyuka kimwili kutoka ardhini pale alipokaa na kuelea hewani (levitate). Tazama mfano HAPA. Wakati mwingine aliweza kutoka nje ya mwili; akauacha mwili wake na kwenda nje huko na kule kufanya mambo mbalimbali (astro-travelling). Na kijana huyu alitumiwa na shetani kuharibu makanisa mengi; na kuwaharibu wachungaji wengi.
Siku moja, alipangiwa kwenda kuharibu kanisa moja ambalo lilikuwa na maombi ya kutosha. Kulitokea na migawanyiko mingi kanisani na kuchanganyikiwa kwingi. Alianza kufanya kazi kwenye kanisa hili; lakini mchungaji wa kanisa lile aliitisha mfungo wa kanisa zima. Kanisa lilipoanza kufunga, watu walitubu sana na kufanya mapatano mengi. Na watu wakawa kitu kimoja, na wakaanza kuomba kwa ajili ya kazi ya Bwana katikati yao. Na wakaendelea kufanya maombezi na kumlilia Mungu ili awarehemu na kuingilia kati maishani mwao. Na kadiri siku zilivyoendelea, bwana huyu alikuwa akija tena na tena akiwa na mapepo kinyume na kanisa hili. Lakini lilitoka neno la kinabii likiwaambia Wakristo wasimame pamoja na kufanya vita dhidi ya nguvu za giza ambazo zilikuwa zinashambulia kanisa lile.
Siku moja, kijana huyu aliuacha tena mwili wake chumbani kwake na akatoka nje. Aliongoza jeshi kubwa la mapepo moja kwa moja hadi kwenye kanisa lile ili kwenda kufanya vita vya kiroho.
Sasa, ufuatao ni ushuhuda wake.
Roho yake ilikuwa inapaa hewani juu ya kanisa lile na kujaribu kulishambulia, lakini kulikuwa na kifuniko cha nuru juu ya kanisa hilo. Wakati waliendelea na mapambano, ghafla, kulikuja jeshi la malaika ambalo liliwashambulia na kukawa na mapambano makali pale hewani. Hatimaye, mapepo yalikimbia, lakini yeye alikamatwa na wale malaika.
Ndiyo, alikamatwa na malaika! Alijiona akiwa ameshikiliwa na malaika sita. Na wakamleta kwa kumpitisha kwenye paa hadi kwenye madhabahu ya kanisa. Akawa yuko pale huku watu wanaendelea kuomba. Walikuwa wamezama kwenye maombi, wakifanya vita vya kiroho; wakifunga na kuvunja, na kutupa nje. Mchungaji alikuwa kwenye madhabahu akiongoza maombi hayo na vita. Roho wa Bwana akaongea na mchungaji, akisema, “Nira imevunjika, na mhusika yuko hapa mbele yako. Msaidie kwa kumfungua.
Mchungaji alipofungua macho yake, alimwona yule kijana akiwa ameanguka pale hajitambui. Mwili wake ulikuwa pamoja naye! Kijana yule anasema kuwa haelewi ni kwa vipi mwili wake uliungana naye; maana alikuwa ameuacha nyumbani. Lakini ndio alikuwa pale; hajui ni kwa vipi aliingia, isipokuwa tu malaika walimpitishia kwenye paa.
Sasa, mambo haya ni magumu kuamini, lakini mchungaji alinyamazisha kanisa na kuwaambia kile ambacho Bwana alimwambia. Kisha akamwuliza yule kijana, “Wewe ni nani?” Kijana yule alikuwa anatetemeka wakati mapepo yalipoanza kumtoka.
Kwa hiyo, waliomba kwa ajili ya kufunguliwa kwake, na hatimaye baadaye alianza kusema ushuhuda wake. Hivi sasa kijana huyu ameshaingia kwa Bwana na ni mwinjilisti, akihubiri Injili. Anatumiwa sana na Bwana kuwaweka huru watu wengine.
Usiku mmoja, mimi (John Mulinde) nilienda kwenye chakula cha usiku mahali fulani. Sababu hasa ya kwenda pale ni kwa vile kuna mtu alinieleza habari za huyo kijana; na nilikuwa na shauku kubwa sana ya kumwona, na kuona kama kweli hadithi yake ina ukweli wowote. Kwa hiyo, nilipofika, nilikaa mezani. Na jioni ile, kijana huyu alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda wake. Alizungumza juu ya mambo mengi sana. Mara nyingine alilia kutokana na mambo aliyoyafanya. Alipomaliza kusema, alitoa ombi.
Kulikuwako na wachungaji wengi pale kwenye ukumbi. Alisema,“Ninawaomba ninyi, wachungaji. Tafadhalini, wafundisheni watu namna ya kuomba.” Watu ambao hawaombi, wanaweza kuchukuliwa na chochote, katika chochote na ibilisi; na ziko hata njia za adui za kutumia maisha yao na maombi yao. Adui anajua hata namna ya kutumia kwa faida yake maombi ya watu wasiojua kuomba. “Wafundisheni watu namna ya kutumia silaha za kiroho ambazo Mungu amezitoa.
Kisha alieleza jinsi ambavyo alikuwa akiongoza mapambano kwenye anga. Alikuwa akienda pamoja na maajenti wengine wa shetani na mapepo mengi hadi angani. Ilikuwa kama zamu. Inabidi kwenda kutekeleza zamu yako. Kwa hiyo, ni mara nyingi tu alikuwa na muda wa kwenda kwenye anga ili kufanya vita. Na akasema kuwa kule angani, kwenye ulimwengu wa roho, kama anga limefunikwa na blangeti la giza, blangeti hilo linakuwa ni nene sana; na ni kama jiwe. Na linakuwa limefunika eneo lote. Na mapepo haya yanaweza kwenda juu yake na chini yake. Na yakiwa huko, yanaweza kuathiri matukio yanayoendelea duniani.
Pale mapepo wachafu pamoja na maajenti wa shetani wa kibinadamu wanapomaliza zamu yao, wanashuka duniani kwenye maeneo ya kimaagano, iwe ni kwenye maji au ardhini, ili kuweza kurejesha upya nguvu zao, maana zinakuwa zimepungua kutokana na kufanya kazi angani wakati wa zamu yao. Na wanarejeshaje nguvu zao? Ni kupitia kafara ambazo watu wanatoa kwenye madhabahu hizi. Kafara zinaweza kuwa ni uchawi wa wazi, damu za aina zote, ikiwa ni pamoja na utoaji mimba, vita, na utoaji wa kafara za wanadamu na wanyama. Zinaweza pia kuwa ni kafara za uzinzi, pale ambapo watu wanafanya uzinzi na uashetati wa kila aina. Na matendo haya maovu yanaleta nguvu kwenye ulimwengu wa giza. Na ziko aina nyingi za kafara.
Kijana huyo alisema kuwa, maajenti wa shetani wanapokuwa juu kwenye anga, na Wakristo wakaanza kuomba hapa duniani, maombi ya Wakristo huonekana kwa namna tatu. Maombi yote huonekana kama moshi ambao unapaa kuelekea mbinguni.
Baadhi ya maombi huonekana kama moshi, na yanaenda juu kiasi na kupotelea hewani. Maombi ya aina hii hutoka kwa watu ambao wana dhambi maishani mwao na hawako tayari kushughulika nazo. Maombi yao ni dhaifu sana, kiasi kwamba yanapeperushwa na kupotelea angani.
nyingine ya maombi nayo ni kama moshi ambao unainuka juu hadi unapofikia kwenye ule mwamba, lakini hayana nguvu ya kupenya mwamba huo. Kwa kawaida, hawa ni watu ambao hujaribu kujitakasa, lakini hawana imani juu ya kile ambacho wanakifanya pale wanapoomba, yaani wanaomba lakini moyoni hawana ujasiri kwamba kile wanachokiomba watakipokea. Mara nyingi huwa wanapuuzia mambo mengine ya muhimu yanayotakiwa wakati mtu anapoomba.
Aina ya tatu ya maombi ni kama moshi ambao umejaa moto. Yanapokuwa yanapaa, yanakuwa ni ya moto sana kiasi kwamba yanapoufikia ule mwamba, unaanza kuyeyuka kama nta. Yanapenya mwamba huo na kuendelea hadi juu.
Mara nyingi watu wanapoanza kuomba, maombi yao huonekana kama aina ya kwanza ya maombi. Lakini kadiri wanavyoendelea kuzama, yanageuka na kuwa ya aina ya pili. Na wakiendelea zaidi, ghafla yanalipuka moto. Na maombi hayo yanakuwa yana nguvu sana kiasi kwamba yanapenya kabisa ule mwamba.
Mara nyingi maajenti wa uovu hubaini kwamba kuna maombi yanabadilika na kuelekea kwenye kuwa moto. Kisha huwasiliana na viumbe vingine vilivyoko duniani na kuwaambia, “Mvurugieni mtu huyo maombi! Mfanyeni aache kuomba! Mwondoeni kwenye maombi!
Mara nyingi Wakristo hushindwa na mbinu hizi. Wanakuwa wanaomba kwa nguvu; wanatubu; wanaruhusu Neno kukagua nafsi zao; imani inaanza kujengeka. Maombi yao yanaanza kuwa na shabaha zaidi. Kisha ibilisi anaona kuwa maombi yao yanaanza kukusanya nguvu. Ndipo vurugu zinaanza ili kuharibu maombi hayo. Mara simu inalia. Wakati mwingine, katikati ya maombi ambapo mtu alikuwa amezama kabisa, , simu inaweza kulia na unawaza kuwa, ngoja niende nikaipokee kisha nitarudi kuendelea na maombi.
Mbinu zingine za kuvuruga maombi nazo zinaweza kutumika; hata kama ni kukugusa mwili wako na kuleta maumivu mahali fulani. Hata pia kukufanya ujisikie njaa ambapo utajisikia kwenda jikoni kutengeneza japo chakula kidogo. Ilimradi tu wakiweza kukufanya utoke mahali pale, wanakuwa wameshakushinda. Wachungaji, ni lazima muwafundishe watu jinsi ya kuomba. Tengeni muda, si tu kwa ajili ya maombi ya juujuu. Mara moja kwa siku, Wakristo wanatakiwa kuwa na muda wa kujielekeza kwa moyo wote kwa Mungu, bila kuwapo kwa kitu chochote cha kuwaharibia umakini wao.
Na kama watu waking’ang’ana kabisa kwa njia hii ya maombi na kuruhusu kupata mwongozo wa kiroho, kisha wakawa wanaendelea na kuendelea, lazima kitu kitatokea rohoni. Moto utalipuka na kugusa ule mwamba na kuuyeyusha! Kuyeyuka kunapoanza, ni moto sana kiasi kwamba hakuna pepo ambaye anaweza kustahimili. Wala hakuna roho ya mwanadamu inayoweza kustahimili pia. Wote wanakimbia.
Kama mtu atajitoa kuomba kwa bidii na kwa kumaanisha namna hiyo, hatimaye kutafuata kufunguka kwa ulimwengu wa roho. Na mara hili linapotokea, matatizo yote haya katika maombi yanafikia mwisho! [Yaani ule ugumu na ule uzito unakwishilia mbali!] Yule ambaye anakuwa anaomba duniani anakuwa sasa anajisikia kuwa maombi ni kitu kilaini kabisa, cha kuburudisha, na chenye nguvu.
Na nimegundua kuwa wakati huo, huwa tunapoteza kabisa hisia za muda na mambo mengine. Si kwamba tunakosa mpangilio; la hasha! Mungu anakuwa anashughulika na muda wetu. Lakini inakuwa ni kama unaachilia kila kitu, na unaunganishwa moja kwa moja na Mungu. Maombi yako yanapopenya, kunakuwa hakuna kizuizi tena kuanzia hapo; na mtu anayeomba anaweza kuendelea kwa muda mrefu kama apendavyo. Hakuna kabisa kizuizi.
Na mara anapomaliza kuomba, lile tundu linabakia wazi.
Kijana huyu pia alisema kuwa, watu wa namna hii wanapomaliza kuomba na kuondoka mahali hapo, lile tundu linakuwa linaondoka pamoja nao. Wanakuwa hawaenendi tena chini ya lile blangeti la jiwe. Wanakuwa wanaenenda chini ya mbingu zilizo wazi. Na akasema kwamba, katika hali hiyo, ibilisi hawezi kufanya kile anachokitaka kwao. Na uwepo wa Mungu unakuwa kama nguzo kutoka mbinguni ikiwa iko juu ya maisha yao. Wanalindwa; na kunakuwa na nguvu kubwa sana ndani ya hiyo nguzo kiasi kwamba kadiri wanavyotembea huku na kule, uwepo huo unakuwa unagusa hata watu wengine. Nguzo hiyo inakuwa inatambua kile ambacho adui amefanya kwa watu wengine. Na pale watakatifu hao wanapozungumza na watu wengine, na wale watu wakawa wamesimama nao, wanaingia ndani ya nguzo hiyo. Na mradi tu wakiwa ndani ya ile nguzo, vifungo vyote vya adui vinadhoofika.
Kwa hiyo, watu hawa wenye mpenyo huu wa kiroho wanapowashuhudia wenye dhambi habari za Yesu Kristo, upinzani wa wenye dhambi unakuwa wa chini. Ni rahisi kuwaleta wenye dhambi kwa Kristo. Wanapoomba kwa ajili ya wagonjwa, au kwa ajili ya mambo mengine, maombi yao yanakuwa na nguvu sana.
Na kama kuna sehemu ambako maombi ya namna hii huombwa mara kwa mara, uwepo wa Mungu unakuja mahali pale na hauondoki. Hivyo, hata watu wasiomjua Mungu wanapokuja kwenye sehemu kama hizo, ghafla vifungo vyao vinakatika.
Na kama atatokea mtu wa kusema nao kwa uvumilivu na kwa upendo, wanaweza kugeuka haraka sana; si kwa nguvu au kwa uwezo, bali ni kwa Roho wa Mungu, ambaye anakuwa yuko pale. Na kama hakuna mtu atakayewajali watu hawa, wanakuja kwenye uwepo wake na kujisikia hatia, wanaanza kujadili kama wakubali au la. Pale watakapoondoka, vifungo vinakuwa na nguvu zaidi kwao. Na ibilisi anajihadi kwa kila njia kutowaruhusu kurudi tena kwenye sehemu kama hizo.
Je, shetani anakaa kimya tu baada ya mtu kupata mpenyo?
Kijana huyu alisema kuwa, ibilisi anawachukia sana watu wa namna hiyo, yaani wale waliopata mpenyo wa maombi.
Sasa unaweza kupiga picha, sote tulikuwa tumekaa chini tunamwangalia kijana huyu akieleza ushuhuda wake. Alikuwa anatueleza mambo ambayo yeye mwenyewe alikuwa akiyafanya na aliyoyashuhudia kwa macho yake. Alitueleza kile ambacho walifanya kwa watu ambao walipata mpenyo katika maombi. Alisema kuwa waliwaweka akilini sana watu kama hao. Kisha waliwafuatilia sana na kujifunza kuhusu wao ili kuwajua vizuri. Walitafuta kila kitu kuwahusu. Hivyo, walifahamu udhaifu wao wote, na ikitokea mtu akawashinda kwenye maombi na kupenya, wanawasiliana na wengine kwenye ulimwengu wa giza na kusema, “Mumlenge mtu huyu kwenye eneo hili na hili. Udhaifu wake uko hapa na hapa.”
Kwa kuwa mtu wa aina hii anapotoka nje ya kifuniko cha maombi, roho ya maombi inakuwa juu yake, uwepo wa Mungu upo juu yake, roho yake inakuwa iko juu, na furaha ya Bwana ndiyo nguvu zake; anapokuwa anaenda, adui anajaribu kila njia kuleta yale mambo ambayo yatamvuruga ili asielekeze macho yake kwa Bwana.
Kama, kwa mfano, imeshajulikana kuwa udhaifu wake uko kwenye eneo la hasira, basi adui atasababisha watu watende mambo ambayo yatamfanya akasirike. Na kama hayuko makini kumsikiliza Roho Mtakatifu, na akaingiwa na hasira, basi ataondoa macho yake kwa Bwana. Na anapokuwa na hasira hivyo, ghadhabu zinamjaa. Baadaye anapokuja kujirudi, anakuwa anataka kutupilia mbali hali hiyo na kuendelea na furaha ya Bwana, lakini anajikuta hajisikii tena ile furaha kama mwanzo. Anajitahidi kujisikia vizuri tena; lakini haiwezekani tena. Kwa nini? Alipojiachilia kwenye kishawishi cha hasira, mapepo walifanya bidii zote katika muda huo kufunga lile tundu kule juu. Na mara waliporudishia lile jiwe, uwepo wa Bwana unakuwa umekatika, yaani ile nguzo iliyokuwa inatokea mbinguni na kumfunika inakuwa haimfikii tena!
Mtu huyo hataacha kuwa mwana wa Mungu. Lakini ule upako wa ziada uliokuwa unaandamana naye maishani; ule uwepo uliokuwa ukitenda mambo bila yeye kutumia nguvu zozote, unakuwa umekatika! Maana pepo wachafu wanatafuta uliko udhaifu wako.
Kama udhaifu wa mtu ni kwenye masuala ya mapenzi, adui ataandaa watu, matukio, na mambo ambayo yatainua hisia za mtu huyo za tamaa ya kimapenzi. Na kama mtu huyo atazikubalia hizo tamaa na kufungua akili yake kuyapokea mambo hayo, na kuyalea nafsini mwake, pale anapomaliza kila kitu na kutaka kurejea tena kwenye hali ya upako ili asonge mbele, anakuta kwamba ule uwepo haupo tena. Labda unasema, “Hii si vizuri kabisa.” Kumbuka tu Biblia inasemaje, “ Tena ipokeeni chapeo ya wokovu. Vaeni dirii ya haki.” Mara nyingi hatuoni haja ya silaha hizi za kivita. Lakini kumbuka Yesu alivyotuambia juu ya namna ya kuomba “Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.”
Kila mara unapopata mpenyo katika maombi, unapofika mwisho, kumbuka kuwa wewe bado ni kiumbe mwanadamu aliye dhaifu. Kumbuka kuwa haujakamilishwa bado. Mwombe Bwana, useme, “Bwana, nimefurahia wasaa huu wa maombi, lakini nitakapotoka nje kwenye dunia, usiniongoze kwenye majaribu. Usiruhusu niangukie kwenye mtego wa ibilisi. Najua kuwa adui anatega mitego kule nje. Sijui ni mitego ya namna gani. Na ninajua kuwa bado mimi ni dhaifu katika baadhi ya maeneo. Kama nikiingia kwenye hali fulanifulani, nitaanguka. Unilinde, Bwana. Unapoona ninaelekea kule ambako kuna mitego niliyotegewa, nifanye nielekee upande mwingine. Uingilie kati, Ee, Bwana. Usiche niende tu kwa nguvu zangu na uwezo wangu. Niokoe na yule mwovu.”
Mungu anaweza kufanya hivyo. Lakini, kama kuna kitu kibaya kitatokea, ambacho kitakufanya uondoe macho yako kwa Kristo, wewe sema tu, “Asante Yesu.” Ndiyo sababu Mtume Paulo aliandika, “Mshukuruni Mungu kwa kila jambo.” Baadhi ya mambo si mazuri. Yanaumiza, na tunashangaa kwa nini Mungu anayaruhusu yatufikie. Lakini kama tu tungejua kwa njia hiyo anatuokoa na mambo yapi, tungemshukuru. Tukijifunza kumwamini Bwana, tutamshukuru kwa kila jambo.
Yule kijana aliendelea kusema kuwa, unapopata mpenyo katika maombi, majibu yako ni lazima yatakuja. Alisema kuwa jibu mara zote huja, lakini mara nyingi, huwa halifiki kwa mtu aliyeliomba. Kwa nini? Ni kwa sababu ya mapambano yaliyoko kwenye anga. Pia, majibu yanaweza kuzuiliwa iwapo viumbe waovu wa rohoni watafanikiwa kurejesha ule mwamba na kuziba tundu ambalo mwombaji alifanikiwa kulitoboa kwa njia ya maombi yake.
Kisha aliongea jambo ambalo kwa kweli lilitikisa imani yangu. Binafsi ilinibidi niingie kwenye mfungo wa siku kumi, ili kumwuliza Bwana kama hilo alilosema lilikuwa na ukweli wowote. Basi sikiliza haya: Kijana huyu alisema kuwa, kila Mkristo anaye malaika ambaye anamtumikia Mkristo huyo. Nasi tunafahamu kuwa Biblia inasema kuwa malaika ni roho wanaotutumikia. (Waebrania 1:14). Alisema kuwa watu wanapoomba, majibu huletwa kwa mikono ya malaika. Malaika huleta majibu, kama ambavyo tunasoma kwenye kitabu cha Danieli. Kisha alisema jambo ambalo ni gumu sana. Alisema kwamba, kama yule anayeomba anafahamu silaha za kiroho na amejivika silaha hizo, majibu nayo huja kwa kupitia malaika ambaye, naye amejivika kikamilifu kwa silaha hizohizo.
Lakini, kama anayeomba hajali silaha za kiroho, basi malaika nao wanakuja bila silaha hizo. Wakristo ambao hawajali kile ambacho kinaingia mawazoni mwao; hawashindani kuangusha mawazo yasiyofaa; malaika wao huja bila chapeo. Silaha zozote utakazoacha kuzitilia maanani duniani, malaika anayekutumikia naye anakuwa hanazo. Kwa maneno mengine, silaha zetu za kiroho hazitulindi miili yetu, bali zinalinda vitu vile vya kiroho tunavyofanikiwa kuvipata kutoka kwa Bwana.
Malaika anapokuwa anakuja, mapepo wanamtazama na kumkagua na kubaini maeneo ambayo hajajifunika; na hayo ndiyo maeneo ambayo watashambulia. Kama hana chapeo kichwani, basi watashambulia kichwani. Kama hana dirii, watashambulia kifuani. Kama hana viatu, watajaribu kutengeneza moto ili kumwunguza miguuni.
Sasa, najua kuwa hili ni gumu kuamini; mimi narudia tu kile ambacho kijana huyu alisema. Kisha tulimwuliza, “Je, malaika wanaweza kuungua moto?” Na unajua alisema nini? Kumbuka kuwa huu ni ulimwengu wa roho. Hizi ni roho kwa roho zinapambana. Mapambano ni makali sana, na pale wanapomshinda malaika wa Mungu, jambo la kwanza wanalokimbilia ni lile jibu alilobeba; na wanalichukua hilo. Na hizi zinakuwa ni zawadi ambazo hutolewa kwa watu kupitia imani za siri, au uchawi.
Kumbuka kile ambacho Biblia inasema kupitia kitabu cha Yakobo. Vipawa vyote vyema hutoka kwa Mungu (Yakobo 1:17). Kwa hiyo, shetani anapata wapi vitu vizuri anavyowapatia watu? Baadhi ya watu ambao hawawezi kupata watoto, huenda kwa wachawi na waabudu shetani, na wanapata mimba! Mtoto anakuwa ametoka wapi? Je, shetani ni muumbaji? HAPANA! Anaiba kutoka kwa watu ambao hawaombi maombi yao hadi mwisho.
Katika Biblia, Yesu alisema, “Ombeni bila kukoma.” Pia alisema, “atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? ” Je, Yesu atakukuta bado unangojea? Au utakata tamaa na kumwacha adui aibe kile ambacho umekuwa ukikiombea?
Na hawaridhiki tu na kuiba jibu la maombi. Wanataka pia kumweka malaika kifungoni. Na wanaanza kupambana naye. Wakati mwingine wanafanikiwa kumkamata na kumfunga malaika. Inapotokea hivyo, Mkristo anakuwa kama chakula chao duniani. Wanaweza kumfanyia chochote maana hana ulinzi tena kwenye ulimwengu wa roho.
Nilimwuliza kijana huyo, “Una maana kuwa malaika anaweza kushikiliwa katika ulimwengu wa giza?” Sasa alikuwa anaeleza uzoefu wake, na akasema, hawatamshikilia malaika kwa muda mrefu kwa sababu ya Wakristo wengine ambao wanaomba mahali pengine. Jeshi la ziada litatumwa, na malaika atakuwa huru. Na kama yule Mkristo anayehusika hajaomba hadi kwenye mpenyo, basi atabakia mateka. Ndipo shetani atatuma malaika wake na malaika wa nuru kwa mtu huyu, na hapo ndipo uongo na udanganyifu unapotokea; maono ya uongo na unabii wa uongo. Uongozi wa uongo, na kufanya kila aina ya maamuzi mabaya. Na mara nyingi, mtu wa namna hii anaweza kupata mashambulizi na vifungo vya kila aina.
Niliondoka kwenye kile chakula cha jioni huku na mawazo mengi sana. Nikasema, “Bwana, sitaki hata kujaribu kuamini jambo hili.” Linaondoa ujasiri na usalama wangu wote! Nilipoenda kumlingana Bwana, ilikuwa ni kwa siku kumi; na Bwana alifanya mambo mawili. Kwanza, si tu kwamba alithibitisha mambo hayo niliyoyasikia kutoka kwa yule kijana, bali pia alifungua akili zangu zaidi ili kuona mambo mengine mengi zaidi ya yale ambayo niliyasikia. Pili, aliniongoza kuona kile ambacho tunatakiwa kukifanya wakati mambo haya yanapotokea ili tuweze kuwa washindi.
Alinipa mambo matatu:
Moja: namna ya kutumia silaha za vita vyetu vya kiroho. Biblia inaziita silaha za Mungu. Si silaha zetu. Tunapozitumia, tunamruhusu Mungu kupigana kwa niaba yetu.
Mbili: tambua uhusiano wa roho zinazotutumikia, yaani malaika, na maisha yetu ya kiroho. Na ni lazima kuwa makini sana na kile kinachotokea mioyoni mwetu; kama mwongozo wa kile ambacho kinatakiwa kutokea rohoni kutuhusu sisi.
Tatu: ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hatakiwi kuja kama mtumishi wetu, kututumikia na kutuletea vitu mbalimbali. Hakimbiikimbii kwa Baba kumweleza kile ambacho tunataka. Hiyo ni kazi ya malaika. Lakini Yeye husimama pamoja nasi. Anafanya nini? Anatuongoza, anatufundisha, anatutangulia, anatusaidia kuomba inavyotakiwa. Na mambo haya yanapotokea kwenye ulimwengu wa roho, anatuambia. Wakati mwingine anakuamsha usiku na kukwambia, “Omba.” Wewe unasema, “Hapana! Muda wangu haujafika.” Na anasema, “Omba sasa!” Kwa nini inakuwa hivyo? Ni kwa sababu Yeye anaona kila kinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho. Wakati mwingine anasema, “Kesho ni kufunga.” Wewe unasema, “Hapana, nitaanza Jumatatu!”
Lakini kumbuka kuwa Yeye anaelewa kile kinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho. Ni lazima tujifunze kuwa makini na Roho Mtakatifu. Anatuongoza kwenye njia za haki. Wapendwa, tuishie hapa. Labda wakati mwingine tutaongea jinsi ambavyo tunaweza kuomba hadi kupata mpenyo, maana sasa tunajua mapambano yaliyoko rohoni na jinsi ya kupenya; na namna tunavyoweza kudumu tukiwa na mpenyo tuliopata. Na mara tunapojifunza hili, linakuwa ni jambo la furaha sana. Tukumbuke tu jambo moja: vita si vyetu, bali ni vya Bwana! Haleluya!
Hebu tusimame. Mwangalie mwenzio machoni na utafakari ni mara ngapi amekosa kile ambacho Mungu alikiandaa kwa ajili yake. Lakini shikaneni mikono kama inawezekana; watu wawili au watatu, kisha tu muambiane, “Hakuna haja ya kushindwa tena! Tunaweza kushinda! Iko nguvu ya kutosha kushinda! Yesu tayari ameshafanya kazi yote.” Muombeane ninyi kwa ninyi ili Bwana aweze kutusaidia kushinda. Hatutakiwi kushindwa. Iko neema ya kutosha; nguvu ya kutosha kuleta ushindi!
Asante Yesu.

Wednesday, November 14, 2012

NOVEMBA CRUSADE YAFANA NDANI YA UKUMBI WA PTA CHINI YA MCHUNGAJI FLORIAN KATUNZI

Ikiwa ni ishara ya siku za mwisho ambapo injili itahubiriwa kwa nguvu na spidi ya ajabu, wiki hili limekuwa la kipekee na la madhihirisho ya nguvu za Mungu zisizo za kawaida. Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake wanamiminika katika kongamano kubwa la maombi na maombezi lililoandaliwa na kanisa la E.A.G.T City Centre chini ya mchungaji wake kiongozi Florian Katunzi katika ukumbi wa PTA uliopo viwanja vya mwalimu JK Nyerere zamani Sabasaba.

Kongamano hilo la siku nane lililoanza siku ya jumapili nakutarajiwa kumalizika jumapili hii linatarajia kupambwa na waimbaji mbalimbali wa gospel nchini wakiongozwa na Bahati Bukuku, Masanja Mkandamizaji, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, Solomon Mukubwa, Madam Ruti, Bonny Mwaitege na waimbaji wengine lukuki zikiwemo kwaya za kanisa hilo.

Ambapo toka jumapili tayari uwepo wa Mungu umeanza kujidhihirisha ukumbini hapo kwa watu mbalimbali kupokea uponyaji na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali vya ibilisi ambapo kwa watu wasiofika katika ukumbi huo wanapata yanayojiri kwakusikiliza Wapo Radio FM inayorusha matangazo ya moja kwa moja kutoka ukumbini hapo.
Ungana nami katika baadhi ya matukio katika picha kama inavyoonekana hapa.
Mchungaji Florian Katunzi akiwaongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar katika maombi.

Solomon Mukubwa kutoka Kenya akiita uwepo wa Mungu katika kongamano hilo.

Solomon Mukubwa akimpiga picha Martha Mwaipaja wakati akiimba.

Martha Mwaipaja wa John Saidi akimtukuza Mungu.

Mchungaji mtarajiwa a.k.a Masanja Mkandamizaji akipiga gombo la uimbaji katika kongamano hilo

Kijana mwenye mavocal Samuel Limbu akimsifu Mungu katika kongamano hilo.

Sio utangazaji tu hata uimbaji ni balaa, anaitwa Silas Mbise ambaye pia ni mtangazaji wa Wapo Radio Fm akimtukuza Mungu katika kongamano hilo,

Mchungaji Yohana Mwegoha akimsifu Mungu. picha kwa hisani ya Yonathanlanda.blogspot.com

Flora Mbasha na mumewe mpenzi Emanuel Mbasha wakimsifu Mungu kwa pamoja.

Eveline Msoome nayeye hakuwa mbali katika kumsifu Mungu.

Picha ya Juu ni Waimbaji Madam Ruth pamoja na Martha Mwaipaja wakiwa na Solomoni Mukubwa kwa Pamoja wakimsikiliza Mtumishi wa Mungu wa Mungu Mchungaji Frolian Katunzi wakati akitamka Neno la Baraka kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.


Umoja wa Makanisa Tanga wasema “hatulidhishwi na Taarifa juu ya uchomaji wa Makanisa”

Waziri wa Mambo ya ndani Mh Dr Emmanuel Nchimbi
 
Baada ya serikali kutoa taarifa yake juu uchomaji makinisa hapa Tanzania. Umoja wa Wachungaji wa Makanisa ya Mkoa wa Tanga umesema hauridhishwi na taarifa zinazotolewa na serikali na viongozi wa siasa kuwa wanaohusika na uchomaji wa makanisa ni wahuni  na si Waislamu wakati wanazuoni na masheikh wa taasisi za kiislamu wanakiri vitendo hivyo vinafanywa na baadhi ya waumini wenzao.
Umoja huo umesema unashangazwa na kitendo Waziri wa Mambo ya Ndani,  Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye naye anavihusisha vitendo hivyo kufanywa na wahuni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwenyekiti wa umoja huo, Dk. Jonathan Mwakimage, alisema serikali inapaswa kushughulikia kiini cha matatizo yanayopelekea kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaowashawishi vijana kufanya vitendo vya kihalifu.
Alisema hawajaridhishwa na namna ambayo serikali imekuwa ikishughulikia wahusika wa vitendo hivyo huku baadhi wakiendelea kuwa na kiburi na kujiona kuwa wako juu ya sheria.
Alisema kumeibuka kundi la watu ambao wamekuwa wakiwashawishi vijana kufanya vitendo vya kuhujumu vitabu vitakatifu jambo ambalo limekuwa likichukuliwa na serikali kama kitu cha kawaida.
“Hapa Tanga kuna makanisa manne yamechomwa moto na taarifa zilifika polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, kuna biblia zilichanwa na kukojolewa mwezi uliopita lakini bado kimya na wahusika wanaendelea kujinadi tu mitaani, sisi haturidhishwi na namna ambayo serikali inachukua hatua,” alisema Askofu huyo.Alisema kuwa umoja huo wa makanisa unalaani vikali kitendo cha kukojolewa kwa Qurani, lakini pia unaona kuwa yule aliyemshawishi mwenzake kufanya kitendo hicho ni mkosaji wa kwanza na anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria sawa na huyo aliyetekeleza  kitendo hicho.
Hata hivyo, aliwaomba maaskofu na wachungaji kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuepuka kulipa kisasi na kuwasihi waumini wao hususan vijana kujiepusha na waovu  wanaowashawishi kukojolea, kuchoma au kuchana Quran.
“Katika hili niwaombe Mashehe, Maimam na viongozi wa kiroho wa dini ya Kiislamu kuwa na msimamo mkali kushughulikia waumini wao kwa kukemea vitendo hivyo kwa wazi ili kudhibiti wenye nia ovu…hii ni pamoja na misikiti inayoendelea kuchochea chuki dhidi ya ukristo na serikali na hasa suala la uchomaji wa makanisa” alisema Dk. Mwakimage.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Canon James Dominic, wa Kanisa la Anglikana, aliitaka jamii kutambua kuwa watu wote wana asili ya tumbo moja kutoka kwa Hawa na Adamu na kwa kutambua hilo Watanzania wanapaswa kuishi kwa umoja, utulivu, amani na upendo.
Alisema ni vigumu kuamini kuwa mtu mwenye dini ya kweli na kumwamini Mwenyezi Mungu kwa dhati anaweza kufanya vitendo hivyo na hasa kwa kutambua kuwa vita ya kidini haina mshindi na ni sumu mbaya kwa usalama wa Taifa.
Umoja huo unahusisha makanisa yote yaliyopo mkoani  Tanga kasoro la Roman Catholic na la Sabato.

Monday, November 12, 2012

WAIMBAJI NA WAIGIZAJI WAZIDI KUOKOKA


Dotnata Posh.
Hizi ni siku za mwisho na YESU yu karibu sana kuja kuchukua au kunyakua kanisa lake. Moja wapo ya ishara kuu ya siku za mwisho iliyonenwa na Yesu mwenyewe katika kitabu cha Mathayo ni Kwamba Injili itahubiriwa kwa kila kiumbe ndipo ule mwisho utakuja. Hivi karibuni kumetokea wimbi kubwa la waimbaji na waigizaji nje ya kanisa wa ndani na nje ya nchi kuamua kuachana na mambo au maisha ya dhambi waliyokuwa wakiishi na kuamua kumrudia MUNGU wao na kujiunga na makanisani.

Hilo limedhihirika nchini kwa waimbaji na wanamuziki kumrudia muumba wao kama ilivyo huko nchini Malawi ambako tunaambiwa waimbaji wengi wameamua kurejea kanisani kumuimbia Mungu kama lilivyoripoti gazeti la Nyasa Times kwamba waimbaji muziki zaidi ya watano wameokoka na kuamua kumwimbia Mungu wao huku wengine wakianzisha na bendi zao kabisa za gospel.

Kati ya waimbaji hao maarufu waliokoka ni pamoja na Sam Sambo, Mlaka Maliro, Phungu Joseph Nkasa, Bon Kavalasanza, Evans Meleka na wengine, ambapo wengi waliozungumza na gazeti hilo wameeleza ninamna gani walivyokutana na Mungu nakuamua kumkabidhi maisha yao.

Kwa upande wa Tanzania waimbaji na waigizaji ambao wameamua kumkabidhi maisha Yesu ni pamoja na Dotnata Posh ambaye ameshatoa wimbo wa gospel na sasa yupo katika masomo ya biblia na kuahidi kufungua kanisa pia aliweka bayana kwamba anampango wa kuwachukua mwimbaji Rehema Chalamila(Ray C), Aisha Madinda ambao amesema wameokoka kwasasa.
Vincent Kigosi (Ray)

Wengine ni Stara Thomas ambaye pia tayari ametoa album ya gospel, wengine ambao walitangaza kuokoka miaka ya karibuni ni pamoja Vincent Kigosi (Ray), Mwanaidi Suka ( Mainda), K- Bazil ambaye kwasasa yupo mkoani Iringa kama mchungaji( kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata), Emanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji ambaye ndoto yake ya kuwa mchungaji amekwishaianza kwa kuhubiri katika mikutano mbalimbali pamoja na wengine wengi.
Stara Thomas.

Swali ni kwa wale waliopo kanisani je wanapokeaje taarifa hizi za wapendwa hawa, je wanachukua jukumu la kuwaombea ama wanachukua jukumu la kuwahukumu?.. ni wajibu wa kanisa sasa kuwalea watu hawa ili wajifunze na waishi maisha ya kumpendeza Mungu.Ni maombi yangu kwamba Mungu wa mbinguni awasaidie wailinde imani ya kweli waliyoipokea hata siku ajapo mwana wa adamu tukamlaki sote mawinguni Amen.
Mwanaidi Suka (Mainda).




Kashumba Bazil (K-Bazil)
Aisha Madinda.                                                                                                                           



Saturday, November 10, 2012

Kenya kubadili sheria ya ndoa

Baraza la mawaziri nchini Kenya linapendekeza mabadiliko makubwa kwa sheria za ndoa nchini humo .Mswaada wawaliowasilisha unapendekeza kuwa wanaume wanweza kuoa zaidi ya mke mmoja na hata kuharamisha mahari ambapo familia ya mwanaume inalipa mahari hiyo.
Wanawake walioolewa Kenya
Pia inataka kuhalalisha watu kuishi pamoja kama mume na mke bila ya ndoa kwa kipindi cha miezi sita kama njia ya kulinda watoto na wanwake wakati uhusiano huo unapovunjika.
Mapendekezo hayo tayari yamezua hisia kali kutoka kwa jamii kwa ujumla. Aidha mswaada huo, lazima uidhinishwe na bunge kabla ya kufanywa sheria.
Wengi wa wanaoishi maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusianao kama huo unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na mume bila ya ndoa.
Wanafunzi hujipata katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma na punde baada ya kuhitimu , huvunja uhusiano ule.
Mara nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za manufaa ya ule uhusiano
Wakati mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja , na hapo ndipo mwanamue hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu yake.
Na hilo ndilo lengo la mswaada huu kulingana na baraza la mawaziri.
Linasema linataka ikiwa utakuwa sheria iweze kulinda akina mama na watoto kutokana na dhulma za nyumbani hususan wanaume wanaokwepa majukumu yao.
Mswaada huu umevutia hisia mbali mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume na tamaduni na desturi za jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari ambalo mswaada huo unapendekeza kutupiliwa mbali.
Dini nyingi kama Uisilamu na hata wahindi wanakumbatia swala na mahari kwa sababu ni matakwa ya dini.
Ingawa baraza la mawaziri limepitisha mswaada huo, inaweza tu kuwa sheria ikiwa bunge litaipitisha. Ikiwa kweli rekodi ya bunge hili ndio itakuwa kigezo cha kupitishwa kwa mswaada huu, bunge lenyewe lenye asilimia hamsini ya wanaume, litatupilia mbali mswaada huo au kuupitisha baada kufanya mabadiliko.
Wengi wa wanaoishi maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusiano kama huo unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na mume bila ya ndoa.
Wanafunzi huishi katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma na baada ya kusoma huachana.
Mara nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za kujinufaisha kwa hali yoyote ile.
Wakati mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja , na hapo ndipo mwanamume hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu yake.
Mswaada huu umvutia hisia mbali mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume na tamaduni na desturi za jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari ambalo mswaada huo unapendekeza kutupiliwa mbali.

Askofu mkuu wa Anglikana ateuliwa rasmi

Askofu mpya wa Anglikana Justin Welby (kulia)

Aliyetangazwa kuwa askofu mkuu wa kanisa Anglikana Cantebery na ambaye amethibitishwa hii leo, Justin Welby amesema ameshangazwa sana na wadhifa aliopewa wa kuliongoza kanisa hilo.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu Justin Welby ambaye ni askofu wa Durham, alielezea msimamo wake wa kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake kama maaskofu.
Aliongeza kuwa watu watu hawapaswi kuwanyanyapa wapenzi wa jinsia moja kanisani, lakini akakiri kuna mgawanyiko kanisani kuhusu ndoa za jinsia moja.
Welby aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta , anaonekana kama mhafidhina kwa mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea upande wa kiivanjelisti. Ataanza kazi yake mwezi Machi mwaka ujao baada ya Askfo mkuu Rowan Williams kuachia ngazi.
Baada ya uteuzi wa Askofu mkuu Justin Welby kuwa mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo wamezungumzia uteuzi huo.
Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Nigeria, Nichola Okoh, ameimbia BBC kuwa uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja usitetewe na Kanisa.

Baada ya matokeo:Amerika imeacha somo gani kwa wakristo?

Rais Barack Obama


Uchaguzi wa Marekani 2012 umemalizika, zaidi ya waamerika 100 millioni walishiriki katika zoezi hili kubwa la kidemokrasia wakitimiza matakwa ya upigaji kura. Hata wakati  zaoezi la kuhesabu halijaisha na michakato mingine ya kiufundi haijakamilika, mwonekano wa ujumla wa uchaguzi ulikuwa wazi, na matokea ya uchaguzi huu kwa hakika ni makubwa na hayatasahaulika kiurahisi miongoni mwa watu wote duniani.
Mambo kadhaa yamejitokeza mara baada ya uchaguzi huu na wakristo kote duniani hatunabudi kuyatafakari kwa kina na kwa makini.

USHINDI WA KUTULIZA
Kwanza, ni lazima tutambue kwamba Rais Barack Obama ameshinda ushindi wa wazi na ulioleta ushwari wa utulivu katika taifa, kura ziliongezeka kwa kasi kufikia zaidi ya 300 kabla ya usiku wa manane. Kinyume cha matarajio ya wengi, ambapo uchaguzi wa 2008 Rais aliunganisha nguvu nyingi pamoja. Kura nyingi kutoka miongoni mwa vijana wa kiamerika, Waafrika-Waamerika, Wahispania, na majimbo mengine muhimu. Mara matokeo ya uchaguzi yalipoanza kutangazwa kimajimbo, ushindi wa Obama ulionekana kiurahi na kwa uwazi kabisa.
Rais Obama akiwa na familia yake baada ya kushinda uchaguzi

Barack Obama aliepuka aibu ya uchanguzi ambayo pia angeshinda kwa kura nyingi. Asili ya kuyatuliza mambo kwa ushindi alioupata umeliokoa taifa na maumivu makali ambayo lingeyapata kwa chaguzi na pointi elfu mbili (2000)  kwa kuleta uamsho na ari mpya katika chama chake. Mambo mengine pia yamekuwa wazi. Uchaguzi umemrudishia na kura zimeonyesha kwamba msimamo wa Rais Obama juu ya swala la ndoa za jinsi moja (same-sex marriage) hauja mgharimu chochote. Hii labda umewashangaza watu wote waliokuwa na misimamo tofauti na wa Rais mteule.
Wakristo sasa hawana budi kumwombea Rais mteule wa taifa kubwa hili. Kama mtume Paulo anavyoelekeza, “Basi kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utaua wote na ustahivu” (1 Tim 2:1-2). Ni lazima tumwombee Rais. Hatuna budi kumwombea afya njema pamoja na familia yake kwa ajili ya stamina na tabia nzuri katika kutimiza majukumu yake ya kila siku. Ni lazima pia tuombee timu nzima ya uongozi ili iweze kuonyesha na kutenda vyema hatimaye iweze kukumbukwa kama ni moja ya timu bora katika historia ya taifa hili.
Wote tunahusika kwa karibu sana. Ni lazima tumwombe MUNGU ili augeuze moyo wa Rais  Obama katika kushughulikia mambo mazito ya taifa hili, hasa kusimamia utakatifu kuanzia maswala ya utoaji mimba mpaka maswala ya heshima ya ndoa yanayosumbua watu wengi hivi sasa. Ni lazima tuende kinyume na kila hali ya uchafu hasa mikakati mbalimbali aliyonayo katika swala zima la njia za kuzuia mimba zilizo kinyume na maadili ya uhuru wa Kidini. Tukiangalia hali yake ya uongozi kwa muhula wake wa kwanza Ikulu (White House), ni lazima tufanye mapema hasa kwa muhula huu wa pili, tukijua kwamba Rais huyu hata shiriki tena katika uchaguzi kwa mujibu wa sheria za Marekani.
Kama Rais alivyodhibitisha katika hotuba yake mara baada ya kuchaguliwa mara ya pili kuwa Rais wa Taifa la Marekani, kwamba Taifa letu linakabiliwa na changamoto kubwa. Hivyo hatunabudi kumwombea Rais ili aongoze katika roho ya umoja wa kitaifa na kuheshimiana, Waamerika wawe wamoja katika kutatua matatizo yao kwa umoja. Majukumu mazito sasa yako begani mwake. Ameshinda mara ya pili kwenda ikulu, sasa ni lazima aongoze kwa haki.
Rais Barack Obama akiwa na makamu wake wa urais pamoja na wake zao

Uchaguzi uliligawa taifa
Asubuhi ilipofika, uchaguzi wa mwaka 2012 ulikuwa hautabiriki kwa vile kura na matokeo yalikaribiana sana kati ya chaguzi zote zilizowahi kufanyika katika historia ya Amerika, saa nane usiku., kura 240,000 tu kati ya zaidi ya 103 millioni zilizopigwa ziliwatenganisha Rais Obama na Govana. Mitt Romney. Tofauti ya  .3% imeufanya uchaguzi huu kuwa wa tatu kwa wagombea kuwa na matokea yaliyokaribiana sana katika historia ya Amerika, akishindwa kwa kura chache sana katika uchaguzi wa 1060 kati ya John F. Kennedy na Richard M. Nixon na uchaguzi wa 1880 kati ya James Garfield na Winfield S. Hancock.
Tofauti za kura za majimbo ni za muhimu sana, lakini kura za wananchi zilionyesha kwa uwazi ni kwa kiasi gani taifa limegawanyika. Taifa limegawanyika kisiasa, lakini yale maswala ya mgawanyiko yameleta pia mgawanyiko katika mataifa yote. Uchaguzi wa mwaka huu (2012) umeweka wazi kwamba Waamerika wamegawanyika juu ya maswali ya msingi. Waamerika wemegawanyika katika kambi zinazoainisha na kuutazama ulimwengu katika mambo kadhaa ya msingi. Ikumbukwe kwamba uchaguzi haukusababisha mgawanyo huu bali umeuibua tu. Mgawanyiko huu katika ngazi ya kimataifa unamfanya Rais Obama kuingiwa na hofu katika kushughulikia changamoto za kisiasa, lakini matatizo na changamoto ni kubwa zaidi ulimwenguni hasa zile za kikanisa/kidini.

Uchaguzi uliobadilika na unaobadilika
Mabadiliko ya kimsingi kwa chaguzi za Amerika yalikuwa dhahiri. Mbadiliko makubwa ya watu namaanisha kuwa uchaguzi uliwa wa kikabila, mila & desturi, na mitazamo iliyotofautiana sana. Uchaguzi umekuwa sio kitu cha kuheshimiwa tena. Tafiti za hivi karibuni zilizofanywa zinaonyesha kuwa kiashirio kimojawapo kikubwa cha upigaji kura ni kiasi cha mahudhurio kanisani/ au kuwa muumini na muhudhuriaji mzuri kanisani. Kwa sasa ni waamerika wachache tu wanaohudhuria makanisani, na utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa 20%  ya Waamerika wote hawana dini yeyote. Hivyo basi kuugeuza uchaguzi kuwa wa kidini zaidi unaweza kuliletea Taifa madhara makubwa na mabaya sana.
Amerika inaendelea kuwa mji, na hili pia limesababisha hali ya upigaji kura. Wapiga kura wapya (vijana) hawajaainishwa kikabila, kwa mtazamo wa muda mrefu chaguzi zinabadilika sana. Waamerika wachache wameoa na ni wachache tu wenye watoto manyumbani kwao. Hili pia, linabadilisha tabia na hali ya upigaji kura. Hizi ni miongoni mwa sababu chache zinazoweza kusababisha mabadiliko ya kimsingi katika Taifa.

Mwisho wa muungano wa warepublican
Ingawaje warepublican wengi wanatiwa moyo kwa kuwa na kura nyingi za uwakilishi, kura za majimbo zitaendelea kukisababishia chama hiki matatizo makubwa sana. Ramani hii haiwaongezei chochote wanarepublicans kwa hali halisi iliopo sasa, bali ni kuibomoa taswira nzima ya chama.  Kwa urahisi niseme hivi, Chama cha Republican hakitaweza kushinda urais kwa sasa mpaka kimebadilika na kuwa ni chama cha vijana wa kiamerika na Wahispanic Amerika. Vinginevyo, kitakuwa ni chama cha kizazi cha wazee waliostaafu wasiopenda mabadiliko. Nafasi ya chama juu wa wahamiaji ni ya hatari sana, na inashangaza hata maadili ya chama chake chenyewe.
Hakuna chama kitakacho shinda kikionekana hakina moyo. Hakuna chama kitashinda kikionekana ni cha weupe na waamerika wazee. Hakuna chama kitashinda kikionekana kinaelekea tulikotoka badala ya kuonyesha njia tunakoenda. Chama cha Republican kisingeweza kushinda kiti cha urais kwa kutumia vigezo vya udhaifu wa uchumi na janga la ukosefu wa ajira, kama mwandishi wa habari George aliweza kusema, chama ambacho hakitashinda kwa mazingira haya ni lazima kitafute namna nyingine ya utendaji kazi.
Chama cha Republican hakinabudi kujitathimini kwa muda wa kutosha na kuiweka sawa taswira na mwelekeo wake. Mchuano huu ni wa muhimu sana, na ni wa maana sana miongoni mwetu tunaothamini na kuhusika sana na mambo kadha wa kadha.

Janga la mmomonyoko wa maadili
Wainjilisti wa Kikristo lazima wautazame uchaguzi huu wa mwaka 2012 katika Taifa hili kubwa la Amerika kama ni janga la kimaadili. Kuchaguliwa kwa Rais Obama unamrudisha Rais anaetetea utoaji mimba katika ikulu ya Marekani (White House), Mapema atakapo pitisha sheria ya kuzikubali ndoa za njinsi moja (same-sex marriage). Rais Obama inawezekana akawa na fursa ya kumteua jaji mmoja au zaidi wa mahakama kuu na kwa uhakika watakubaliana juu ya falsafa ya katiba ya Nchi.
Zaidi ya hapo, majimbo mawili, Maine and Maryland, yalihalalisha ndoa za jinsi moja. Jimbo la Washington pia liko mbioni kuhalalisha mpango huo. Juhudi za kufanya marekebisho ya kuzuia ndoa za jinsi moja ziligonga mwamba katika jimbo la Minnesota. Hii ilikuja mara baada ya majimbo 33 kupitisha ainisho la ndoa kama ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke. Mara baada ya ushindi huu wa majimbo 33, usiku wake majimbo kadhaa yalitangaza kujitoa na hivyo kukubaliana na kuhalalisha ndoa za jinsi moja, majimbo haya ni Maine and Maryland (na labda Washington) yakawa ni majimbo ya kwanza kuhalalisha muunganiko wa ndoa za jinsi moja kwa kupiga kura.
Kwa uwazi kabisa, tunakabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili hapa Amerika, na changamoto kubwa zaidi miongoni mwetu tunaojali na wenye wivu juu ya maswala haya. Tunakabiliana na changamoto ya dunia nzima ambayo ni kubwa zaidi ya changamoto ya kisiasa, ni lazima tujifunze kuwashawishi waamerika katika kushirikishana hukumu za dhamira zetu za kimaadili juu ndoa, jinsi na utakatifu wa maisha na mambo kadhaa ya kimaadili. Hii haiwezi ikawa ni jambo rahisi. Lakini linahitaji mwitikio wa pamoja na haraka katika kulishughulikia.

Sio tu kuhusu siasa
Wakristo hawapaswi kuona vitendo vya kisasa kama ndio mwisho wa mambo, bali tu ni kama mwanzo na njia. Hatuwezi kutafuta wokovu kupitia mabox ya kura pekee, na kamwe tusimtegemee masia wa kisiasa. Wakristo lazima wachukue wajibu wa kisiasa, kusimika upendo wa Mungu na katika kuwapenda majirani. Sisi tunhusika sana na ulimwengu huu, japo ni kwa kiasi Fulani tu. Lengo letu kuu ni Injili ya Yesu Kristo.
Kuishi katika ulimwengu lakini tukiwa sio wa ulimwengu huu haijawahi kuwa rahisi. Uchaguzi huu wa Amerika umeainisha changamoto tunazo kabiliana nazo sasa na wajibu tunaotakiwa kuufuata na kuutenda.
Kwan nchi za ulimwengu wa tatu na zinzoendelea zina kila sababu ya kujifunza kwa yote yanayotokea katika mataifa makubwa kama Amerika. Wakristo pia lazima wawe macho kuhakikisha kwamba mpango wa Mungu unasimama. Tusipoomba Mungu, wanawake waombolezaji wasiposimama na kuliombea taifa. Mambo mabaya kama ndoa za jinsi moja zitafika mpaka huku kwetu na zitaingia mpaka makanisani haya makanisa ya Kipentekoste.Ni wajibu wetu kama watu wa Mungu kuomba Mungu kwa bidii tukipambana na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho.