Wednesday, November 14, 2012

NOVEMBA CRUSADE YAFANA NDANI YA UKUMBI WA PTA CHINI YA MCHUNGAJI FLORIAN KATUNZI

Ikiwa ni ishara ya siku za mwisho ambapo injili itahubiriwa kwa nguvu na spidi ya ajabu, wiki hili limekuwa la kipekee na la madhihirisho ya nguvu za Mungu zisizo za kawaida. Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake wanamiminika katika kongamano kubwa la maombi na maombezi lililoandaliwa na kanisa la E.A.G.T City Centre chini ya mchungaji wake kiongozi Florian Katunzi katika ukumbi wa PTA uliopo viwanja vya mwalimu JK Nyerere zamani Sabasaba.

Kongamano hilo la siku nane lililoanza siku ya jumapili nakutarajiwa kumalizika jumapili hii linatarajia kupambwa na waimbaji mbalimbali wa gospel nchini wakiongozwa na Bahati Bukuku, Masanja Mkandamizaji, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, Solomon Mukubwa, Madam Ruti, Bonny Mwaitege na waimbaji wengine lukuki zikiwemo kwaya za kanisa hilo.

Ambapo toka jumapili tayari uwepo wa Mungu umeanza kujidhihirisha ukumbini hapo kwa watu mbalimbali kupokea uponyaji na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali vya ibilisi ambapo kwa watu wasiofika katika ukumbi huo wanapata yanayojiri kwakusikiliza Wapo Radio FM inayorusha matangazo ya moja kwa moja kutoka ukumbini hapo.
Ungana nami katika baadhi ya matukio katika picha kama inavyoonekana hapa.
Mchungaji Florian Katunzi akiwaongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar katika maombi.

Solomon Mukubwa kutoka Kenya akiita uwepo wa Mungu katika kongamano hilo.

Solomon Mukubwa akimpiga picha Martha Mwaipaja wakati akiimba.

Martha Mwaipaja wa John Saidi akimtukuza Mungu.

Mchungaji mtarajiwa a.k.a Masanja Mkandamizaji akipiga gombo la uimbaji katika kongamano hilo

Kijana mwenye mavocal Samuel Limbu akimsifu Mungu katika kongamano hilo.

Sio utangazaji tu hata uimbaji ni balaa, anaitwa Silas Mbise ambaye pia ni mtangazaji wa Wapo Radio Fm akimtukuza Mungu katika kongamano hilo,

Mchungaji Yohana Mwegoha akimsifu Mungu. picha kwa hisani ya Yonathanlanda.blogspot.com

Flora Mbasha na mumewe mpenzi Emanuel Mbasha wakimsifu Mungu kwa pamoja.

Eveline Msoome nayeye hakuwa mbali katika kumsifu Mungu.

Picha ya Juu ni Waimbaji Madam Ruth pamoja na Martha Mwaipaja wakiwa na Solomoni Mukubwa kwa Pamoja wakimsikiliza Mtumishi wa Mungu wa Mungu Mchungaji Frolian Katunzi wakati akitamka Neno la Baraka kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment