Ni
takribani wiki tatu mfululizo Mchungaji Dr. Ezekiel Mbwilo wa kanisa la TAG
Kijitonyama (mwangalizi msaidizi wa section ya Kinondoni) amekuwa na somo la
Roho mtakatifu. Roho mtakatifu ni wa muhimu sana katika kanisa na katika maisha
ya mwamini. Yesu aliona umuhimu wa Roho mtakatifu ndo maana akasema, hainabudi
mimi kuondoka ili aje yule Roho mtakatifu akae kwenu, naye atawafundisha kweli
yote. Somo hili ameligawa katika vipengele vingi, kipengele cha kwanza kilikuwa
“Umuhimu wa Roho mtakatifu” ambapo alianza kwa kufundisha majina mbalimbali ya
Roho mt. Ikifuatiwa na alama/viwakilishi vya Roho mtakatifu.
Katika
wiki hii (jumapili hii) Mtumishi wa Mungu aliendeleza somo hili kwa kichwa
kinachosema “KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU”
Akihubiri
hapa kanisani Mch.Dr. Mbwilo alisema, Karama ni vitendea kazi kutoka kwa Mungu
kwenda kwa mwamini kwa ajili ya kufanya kazi ya Mungu. Zipo karama tisa (9) za
Roho mtakatifu 1Korith. 12:7-11. Ili kuzielewa vizuri karama hizi, muchungaji
alizigawa katika makundi makuu matatu (3) kama ifuatavyo:-
1.Karama mafunuo ambazo ni
a. Neno la Hekima
b. Neno la maarifa
c. karama ya kupambanua Roho
2. Karama za Nguvu
a. Imani
b. Karama za miujiza
c. karama za uponyaji
3. karama za Lugha
a. Unabii
b. Aina za lugha
c. kutafsiri lugha
Karama hizi si kwaajili ya Mchungaji au
wazee wa kanisa pekee yake bali ni kwa ajili ya kila mwamini.
A.
KARAMA
ZA MAFUNUO
(1) Neno la hekima; Huu ni ufunuo wa Mungu
kwa ajili ya kushughulikia tatizo fulani (mdo 6:1-5; 15:1-15; 1wafalme
3:16-27). Hivyo tunahitaji neno la hekima ili kutatua matatizo yanayotukabili. Karama
hii haileti vinyongo, magomvi bali huleta amani, umoja na mapatano. Karama hii
pia inasaidia kulielewa neno la Mungu, na inasaidia kujua mambo yajayo. Mfano
ufunuo wa Mungu kwa Nuhu juu ya hukumu ya dunia, hivyo kuchukua mtu kuchukua
hatua stahiki. Pia inatusaidia kujua mapenzi ya Mungu na mawazo ya Mungu katika
maisha yetu.
(2) Neno la maarifa: karama hii humfunulia
mtu kuhusu ukweli au mambo yaliyofichika. Pia inasaidia kuelewa yale yanayo
endelea kwenye akili za mwingine mfano ni ile habari ya Anania na Saphira Mdo
5:1-10. Huweka wazi mambo ya siri ya ndani
yaliyofichika kwa wengine. Mfano mzuri ni habari ya mwanamke msamaria
Yohana 4:16-19 na habari ya Gehazi na Elisha 2wafalme 5:20-27
(3) Karama ya kupambanua Roho: Inasaidia
kujua ni Roho gani inafanya kazi katika mtu: Je ni roho ya mtu, au ibilisi au
Roho ya Mungu (Mdo 8:18-24;13:6-12. Tunahitaji karama hizi ili tuweze
kumtumikia Mungu vizuri.
Mpenzi msomaji somo hili
litaendelea wiki ijao usipitwe, temebelea blog hii mara kwa mara uweze
kufaidika kiroho na kimwili pia. Ebu angalia matukio ya ibada katika picha hapa
chini.
Wapendwa wakibubujika ibadani |
Mama grace akiwa kazini ibadani akiongoza kusifu na kuabudu |
waumini wa TAG kijitonyama wakimwabudu Mungu |
Kikundi cha kusifu na Kuabudu kikiwa kazini |
Watu wakibubujika katika ibada |
Kijitonyama Anointed Singers wakiimba kanisani |
Mzee wa zamu(kulia) akiwa na mtafasiri wake wakati wa matangazo |
Mch.Dr. Mbwilo (kulia) akihubiri na mtafasiri wake |
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMatakatifu mwenye NGUVU KUTUONGOZA.
Delete