Leo ni siku ya
pili ya semina, ambapo mtume Israel akiwa na ujumbe maalumu kwa ajili ya
Tanzania na kanisa la Tanzania.
Alisisitiza,
ili mtu afikie na afanye kile kitu Mungu amempangia katika maisha ni lazima
wawepo watu wa kumsaidia.Kwa ufupi ni kwamba kuna mtu ana muujiza wako, na siku
mtakapo kutana utapata muujiza wako. Hii ina maana kwamba ili wewe ujue na
kutimiza lengo la kwa nini upo duniani ni lazima wawepo watu watakao kusaidia
kufikia lengo lako. Kwa bahati mbaya watu wengi hawajui kwamba wanatembea na
miujiza ya watu wengine hivyohivyo watu wengi hawajui ni nani mwenye muujiza
wake/wao. Kitendawili hiki utakitegua kwa maombi tu. Ni maombi yangu leo Mungu
akukutanishe na mtu mwenye muujiza wako.
Akihubiri
katika ibada ya jumatatu jioni, mtume Israel akiwa na ujumbe usemao “Msaidizi wa kukusaidia ufikie hatma yako” alisoma
katika biblia kitabu cha Yohana 2:2 inayohusu Yesu katika harusi ya kana. Ukiwa
ni muujiza wake wa kwanza, aliufanya kwa sababu mama yake ni kama
alimlazimisha. Baada ya harusi ile kutindikiwa divai, mama yake Yesu (mariamu)
alimwambia Yesu kwamba Divai imeisha, Yesu alimjibu mama yake “nina nini na
wewe mwanamke? Tukiangalia hapa hili jibu lilionyesha Yesu hakupenda kufanya muujiza
kwa sababu muda wake ulikuwa haujafika. Cha muhimu hapa ni kwamba mwisho wa
siku Yesu alifanya muujiza wa kugeuza maji kuwa divai safi na njema. Hapa
tunaona mariamu aligundua kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kufanya muujiza.
Hivyo alimsaidia Yesu kuanza kufanya miujiza. Sisi leo tunahitaji watu kama
mariamu watakao weza kutusaidia kugundua kile kitu tunatakiwa kufanya katika
maisha yetu. Ndugu yangu unahitaji mtu akusaidie ufikie leongo lako.
Akihubiri huku
mahubiri yakiambatana na maombi alisema kwa kutumia mifano mingi kutoka katika
Biblia, Mungu alimwambia Musa atafute watu 70 kwa ajili ya kumsaidia afikie
lengo katika maisha kupitia huduma aliyokuwa anaifanya. Esta alimuhitaji
Mordekai ili afike ikulu Esta 5:6-8. Wakati wana wa Israeli wakiwa vitani Musa
alihitaji watu wa kumsaidia kuitegemeza mikono yake ili israeli ishinde vita,
hivyo Haruni na Huri wakaitemeza mikono ya Musa na ushindi wakaupata.
Ndugu yangu
msomaji najua unatamani sana kufikia lengo katika maisha yako. Ili haya yatimie
unahitaji Mungu akuunganishe na watu wenye miujiza yako, na watakao kusaidia
ufikie lengo. Ebu tenga muda wa maombi ili Mungu akuongoze kukutana na watu
hao. Mungu akubariki sana sana.
Mtume Eric Israeli akisikiliza ushuhuda wa mama aliyeponywa na uvimbe tumboni |
Watu wengi wakiwa wamejiandaa kutoa ushuhuda wa mambo makubwa Mungu amefanya |
Kwaya ya Kijitonyama Anointed wakiimba kanisani |
Hapa kila mtu alikuwa anapokea toka kwa Mungu wakati wa maombezi |
Mtume Israeli na Mch.Dr. Mbwilo wakiombea watu wenye shida Mbalimbali wakati wa semina |
Ibada hii ya leo iliambatana na huduma ya kinabii ambapo watu wengi walibarikiwa sana tena sana.
Mpenzi msomaji wangu usikose ibada kama hii kesho,Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele.