Vitu
vingine huonekana na kusababisha hisia za woga, na kutahadharisha. Ebu chukua
mfano wa nyoka. Kwa watu wengi, nyoka mara zote hubeba na kuonekana kama ishara
ya uovu na hatari. Mimi binafsi siwapendi nyoka. Hutemebea taratibu kwa
kujifuta ili wasisikiwe na watu. Kama ungeweza kuniuliza kwa nini, kuna sababu
nyingi na nzuri hapa: macho yao madogo ya mduara, matendo/mwendo wao wa
kitahadhari, mwendo wao usiogundulika kirahisi, ngozi zao nyororo na zenye
utelezi(ndio, najua , magamba)… mwendo wao wa kiupandeupande, na mara zote
huonekana wako tayari kushambulia yeyote mbele yao. Lakini kama mwendo na
uhatari wao ndo unawafanya kuwa waovu, kwa nini isiwe papa, buibui au hata
simba?
Naamini
tunaweza kupata jibu zuri kutoka katika bustani za Edeni. Shetani, baada ya
kumwasi Mungu na kufukuzwa mbunguni, alichagua kujificha kwa umbo la nyoka. Ikiwa
ni matokeo, maelfu ya miaka baadae, bado tunahusisha nyoka na uovu kwa umbo
lake la asili.
Nilikuwa
nasoma kitabu cha Yakobo ghafula
nikamwelewa nyoka kwa njia ya tofauti sana, baada ya ufahamu ulionijia
kwa mfano wa ubaya zaidi ya ulivyofafanuliwa. Kaika Sura ya 3, Yakobo
anawahusia wakristo watambue umuhimu wa kuwa makini na maneno yao/kulinda ndimi
zao. Alifafanua ulimi wa mwanadamu ni kama:
“...Haujatulia
na muovul, umejaa sumu.” (Mstari wa 8)
Lakini
unakuwa mbaya zaidi:
“Mara
nyingine[ulimi] humsifu Bwana na Baba yetu, na mara zingine tunautumia kuwa
laani wote walioumbwa kwa mfano wa Mungu.” (Mstari wa 9)
Je
ulishafanya hivyo? Mimi najua nisha wahi kufanya hivyo.
“Na
ndivyo baraka na laana zinatoka kwenye kinywa kimoja.” (Mstari wa 10a)
Mara
baada ya kusoma mstari huo, sura ya ndimi mbili ndefu za nyoka nilizozitafakari
katika mawazo yangu. Biblia inaeleza na kufafanua juu ya mahubiri mabaya kwa
njia hii: “Usengenyaji, kuwadharau wengine, kujisifu, kuwanyanyasa wengine, walimu
wa uongo, malalamiko na uongo.” Kwa bahati nzuri kila mtu anajua ni mara ngapi
ameutumia ulimi wake vibaya akidhani kwamba Mungu hamuoni.
Ni
rahisi sana kuufikiria uovu kama uasi, ukali, na wenye sumu kali. Shetani akiwa
mwenye ghadhabu na hasira nyingi baada ya kufukuzwa mbinguni, alimwendea Adam
na Hawa kwa umbo la Nyoka bila kuogopa. Kwa ujanja mwingi akitumia maneno
mazuri yaliyojaa wingi wa ushawishi, huku akiwa amejaa hasira, kinyongo na wivu
wa kutaka kumharibu na kumnyang’anya mwanadamu mamlaka aliyopewa na Mungu.
Shetani alifanya kwa urahisi kabisa, hakutumia silaha ,uchawi, mazingaumbwe
wala nguvu. Alichofanya shetani ni kidogo sana, alitumia silaha ndogo na
inayodharauliwa na wengi, “ULIMI”. Kwa ulimi, Shetani aliweza kumjaribu Adam na
Hawa kwa swali moja na rahisi,
“Eti
Mungu amesema…” (Mwanzo 3:1b)
Kama
wakristo, tunafanya kila iliyo juhudi kujilinda na aina zote za uovu. Mauaji, Uzinzi,
wizi… lakini bado, tumeshindwa kugundua kwamba kinachotoka vinywani mwetu
vinauwezo mkubwa wa kutuletea maumivu, kutujeruhi…na ndiyo, hata kifo.
“Chochote
kiujazacho moyo wako ndicho ukisemacho…kwa sababu ndani ya moyo wa mwanadamu
hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, aina zote za uasherati, wizi, usengenyaji,
na uongo.” (Mathayo 12:34, 15:18-19)
Tunajilindaje
wenyewe na “umbea, kuwadharau wengine, na
walimu wa uongona uongo?” Biblia inasema juu ya yote,
“Linda
sana moyo wako, maana ndiko zitokako chemichemi za uzima.” (Mithali 4:23)
Swali
linabakia, Je mtu anawezaje kuulinda moyo wake? Ni kwa kuyakumbuka na kuyatenda
yote aliyoyaamuru Mungu na kwa kuwa tayari kufunikwa na nguvu za nane lake
kinyume na mipango miovu ya shetani,
“Moyoni
mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi.” (Zaburi 119:11)
No comments:
Post a Comment