Ndugu
zangu watanzania, napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole Wakristo wote kwa yote
yaliyotokea mbagala na kwa uharibifu mkubwa uliofanywa wa nyumba za ibada
(makanisa). Najua inauma sana na imeleta usumbufu mkubwa sana miongoni mwetu. Mbali
na yote namshukuru Mungu wa Bwana wetu Yesu atupae amani na subira hasa
tunapopita katika matatizo makubwa kama haya. Ni maombi yangu kuwa, Mungu wa
Bwana wetu Yesu Kristo aendelee kutupa amani, furaha na upendo kwa mapito yote
tupitiayo.
Tunapoona haya yote
yanatokea, naomba niwakumbushe wakristo wenzangu vitu kadhaa katika misingi na
imani ya Kikristo;-
v Kushindana kwetu sii juu ya damu na nyama bali ni
katika falme na pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Waefeso 5).Huu ni wakati
wa Kumwomba Mungu na wala si wakati wa kupambana na katika damu na nyama.
Katika hali isiyoyakawaida, kuna vitu vingi sana vinaendelea katika ulimwengu
wa roho(usioonekana). Unachokiona kinatokea au kinafanyika katika ulimwengu huu
unaooneka kimeanzia katika ulimwengu unsioonekana (ulimwengu wa roho).Wakristo
wanajua siri hii, hivyo ni wito wangu kwamba, twende katika maombi na tumwite
Mungu, na tuharibu kila utendaji na hasa wimbi hili la uharibifu linaloendelea
katika nchi yetu. Najua na nina uhakika kwamba litakoma katika jina la YESU.
v Ukristo umejengwa katika msingi thabiti na imara ambao
ni YESU mwenyewe. Yesu alikuja duniani kumuokoa mwanadamu aliyekuwa amepotea katika
dhambi ili amuweke katika ufalme wake. Katika harakati zake za kumuokoa
mwanadamu, Yesu hakutumia upanga wala hakumwaga damu. Yesu aliwapenda na
anawapenda watu wote. Anawapenda adui zake,na aliwaombea( Mathayo 6,7,8,9).Huu
ni mfano mzuri wa kuigwa na wakristo
wote duniani.Pamoja na yote yaliyotokea mbagala, na mabaya yote wanayotendewa
wakristo, ni muhimu tukapata msaada wetu toka kwa Mungu. Kulipiza kisasi si juu
yetu, Biblia inasema kisasi ni juu ya Mungu mwenyewe.
v Kunajambo Mungu anasema na kanisa la Tanzania: wakati
huu ambapo tumeshuhudia makisa saba (7) yakichomwa na Waislamu Dar es salaam,
Mbagala na mengine yaliyochomwa Zanzibar, na Mwanza. Bila shaka Mungu anasema
kitu, na anataka atufundishe kitu fulani.Ni maombi yangu kuwa Mungu aseme nasi,naomba
kanisa la Mungu Tanzania, litege masikio yake lipate kusikia na kuona kile
Mungu anafanya Tanzania.Hakuna kitu ambacho kinaweza kutendeka duniani pasipo
Mungu kuwajulisha watumishi wake. Naomba wakristo wenzangu tumwombe Mungu, wako
wapi wanawake waombolezaji, nawajitokeze sasa wakaomboleze juu ya Taifa la
Tanzania, Juu ya wamama,watoto, wababa, wazee na vijana wa Tanzania.
v Maombi na subira ndiyo silaha yetu: napenda
niwakumbushe wakristo wenzangu kwamba,sisi tunajivunia maombi silaha yetu ya
ushindi.Kwa mkristo yeyote na mahali popote alipo lazima atambue kuwa huu ni
wakati wa maombi na wala si maneneo tu yasiyokuwa na tija. Kupitia maombi
tunaweza kutuliza dhoruba na hali ikawa shwari. Namwamini Mungu anaweza
kutuliza hali, na amani ikaendelea kudumu katika Taifa letu. Hii itawezekana tu
endapo ufahamu huu utawaingia Wakristo na wakaingia kwenye maombi ya
kudhamiria. 2 Nyakati 7:14) inasema ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina
langu....................nitasikia toka juu mbinguni nitasamehe dhambi yao na
kuiponya nchi yao.
Naomba
niwasihi watanzania na wakristo wote Tanzania kuwa na subira na kumwachia Mungu
awatetee katika yote wanayopitia.Hakuna mtu aliyeamua kumtegemea na kumwamini
Mungu kwa dhati, halafu mwisho wa siku akaaibika au Mungu akamwacha mtu huyo,
haiwezekani.
|
POLISI WAKIWASHIKA BAADHI YA WALIOSHIRKI KATIKA VURUGU |
|
VITU VIKIWA VIMECHOMWA BARABARANI |
|
MOJA LA GARI LA POLISI KATIKA KUWADHIBITI WAANDAMANAJI |
|
POLISI WAKIDUMISHA USALAMA KATIKA ENEO LA TUKIO |
|
MOJA KATI YA MAKANISA SABA LIKICHOMWA MOTO |
|
WAISLAMU WAKIWA KITUO CHA POLISI WAKIDAI WAPEWE MTUHUMIWA WAO |
|
MLANGO WA KANISA UKIWA UMEHARIBIWA KWA MAWE |
|
WACHUNGAJI NA WAUMINI WAKIANGALIA UHARIBIFU ULIOFANYWA KANISANI |
|
MABENCHI YA KANISA YAKIWA YAMEVUNJWA KABISA |
|
MABENCHI YAKIWA YAMEVUNJWAVUNJWA |
|
MIMBARI IKIONEKANA KUCHOMWA MOTO KABISA |
|
HUU NI UHARIBIFU MKUBWA |
|
BAADHI YA VYOMBO VYA MUZIKI VIKIWA VIMEUNGUZWA |
|
MADIRISHA NA MILANGO IKIWA IMEHARIBIWA KABISA |
|
OFISI YA MCHUNGAJI IKIWA IMEHARIBIWA KABISA |
|
BAADHI YA WACHUNGAJI WAKISUBIRI TAARIFA KUTOKA POLISI |
|
BAADHI YA WAUMINI WAKIOMBA MUNGU |
|
VYOMBO VYA MUZIKI VIKIWA VIMECHOMWA MOTO |
|
WAUMINI WAKITAFAKARI KILICHOTOKEA KANISANI KWAO |
|
MOJAWAPO LA GARI LILILOHARIBIWA VIBAYA KABISA |
|
KUSHOTO NI MSIKITI AMBAO WAISLAMU WALIJIKUSANYA NA KULIVAMIA KANISA UPANDE WA KULIA NA KUFANYA UHARIBIFU MKUBWA |
No comments:
Post a Comment