Wednesday, October 17, 2012

MATAMKO MBALIMBALI YAZIDI KUTOLEWA KUHUSU UCHOMAJI MAKANISA NA VIONGOZI WA DINI



ASKOFU MWASOTA

Maaskofu na wachungaji wa umoja wa makanisa ya kipentecoste (PCT) wameitaka serikali kuchukua hatua madhubuti kutokomeza wimbi la uchomaji wa makanisa sambamba na uharibifu wa mali, kwa hali hiyo inaweza kusababisha kupoteza amani nchini.

Kauli hiyo imetolewa na viongozi hao katika kikao chao walichofanya katika kanisa la Naioth Gospel Assembly lililopo mabibo external jijini Dar es salaam ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao hicho, katibu mkuu wa PCT askofu David Mwasota amesema kuwa kikao chao hicho kimefanya tathimini wa kinachoendelea nchini huku serikali ikiona kuwa kukojolea msaafu ndiyo kosa kubwa kuliko mengine.

Aidha amesema kuwa kauli ambayo imetolewa na Rais Kikwete ya kuwataka wakristo kuviachia vyombo vya dola suala hilo, kuwa ni nyepesi sana kulingana na matukio ya kuchoma madhabahu, askofu Mwasota ameyataka makanisa kulinda majengo yao na mali zao kwa namna yoyote watakavyoweza kwani serikali imekwishapewa taarifa.

Amesema kuwa viongozi wa nchi hii ni waislamu ambao mara nyingi huabudu kwenye misikiti ambayo matangazo mengi hutolewa misikitini juu ya kuwadhuru wakristo na viongozi wakipewa vidhibiti lakini hawachukui hatua.(taarifa hii ni kama ilivyoripotiwa na gospelkitaa blog).


Sisi maaskofu na viongozi wa makanisa ya kikristo kutoka CCT, TEC na PCT baada ya kusikia na kuona katika vyombo vya habari juu ya uvamizi wa makanisa tumechukua fursa ya siku hii ya leo ili;-

     1)Kujionea wenyewe madhara yaliyotokea
     2)Kutoa pole kwa waumini wetu
     3)Kushiriki pamoja uchungu wa madhara yaliyotupata
     4)Kuwepo kwa pamoja namna ya kukabiliana na uvamizi huo

Baada ya kutembelea maeneo yaliyovamiwa na kujionea uharibifu uliotokea:-
     1. Tumeona uchungu na masikitiko ya kwamba watanzania tumefikia
         kiwango hicho cha kumtendea jirani  yake 
    2. Tunatambua subira na uvumilivu mkubwa uliooneshwa na wakristo
        kuepusha majibizano ambayo yangeweza kuleta athari kubwa zaidi.
    3. Tumeziona juhudi za jeshi la polisi katika kudhibiti hali ya vurugu na
       kuepusha kupoteza uhai wa raia.

Katika wakati huu:- 

     1. Tunawaalika wakristo wote kutolea sala na maombi kwa Mungu aliye
         mlinzi wetu,usalama na ulinzi wetu uko mikononi mwa Mungu pekee.

     2. Tunatambua kuwa usalama wa wafuasi wa Kikristo ni haki ya msingi
         kama raia wengine wowote, ni mategemeo yetu kwamba wakristo na
        nyumba zao za ibada vinastahili kuhakikishiwa usalama.

Tunapenda kuwaambia Wakristo wenzetu kwamba kikao chetu cha leo kimetupa fursa ya kujionea wenyewe hali halisi ya uvamizi, kwasasa tunajiandaa kuchukua hatua muafaka. Tutawarudia hivi karibuni mbele ya vyombo husika yale yaliyo maamuzi yetu.

Kwa wakati huu tunawaomba muendelee kuwa wavumilivu na watulivu na muwe macho katika kulinda mali na nyumba zetu za ibada kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

Tunawapa pole wote na kuwatakia Baraka za Mungu.


No comments:

Post a Comment