Wednesday, October 17, 2012

MATAMKO MBALIMBALI YAZIDI KUTOLEWA KUHUSU UCHOMAJI MAKANISA NA VIONGOZI WA DINI



ASKOFU MWASOTA

Maaskofu na wachungaji wa umoja wa makanisa ya kipentecoste (PCT) wameitaka serikali kuchukua hatua madhubuti kutokomeza wimbi la uchomaji wa makanisa sambamba na uharibifu wa mali, kwa hali hiyo inaweza kusababisha kupoteza amani nchini.

Kauli hiyo imetolewa na viongozi hao katika kikao chao walichofanya katika kanisa la Naioth Gospel Assembly lililopo mabibo external jijini Dar es salaam ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao hicho, katibu mkuu wa PCT askofu David Mwasota amesema kuwa kikao chao hicho kimefanya tathimini wa kinachoendelea nchini huku serikali ikiona kuwa kukojolea msaafu ndiyo kosa kubwa kuliko mengine.

Aidha amesema kuwa kauli ambayo imetolewa na Rais Kikwete ya kuwataka wakristo kuviachia vyombo vya dola suala hilo, kuwa ni nyepesi sana kulingana na matukio ya kuchoma madhabahu, askofu Mwasota ameyataka makanisa kulinda majengo yao na mali zao kwa namna yoyote watakavyoweza kwani serikali imekwishapewa taarifa.

Amesema kuwa viongozi wa nchi hii ni waislamu ambao mara nyingi huabudu kwenye misikiti ambayo matangazo mengi hutolewa misikitini juu ya kuwadhuru wakristo na viongozi wakipewa vidhibiti lakini hawachukui hatua.(taarifa hii ni kama ilivyoripotiwa na gospelkitaa blog).


Sisi maaskofu na viongozi wa makanisa ya kikristo kutoka CCT, TEC na PCT baada ya kusikia na kuona katika vyombo vya habari juu ya uvamizi wa makanisa tumechukua fursa ya siku hii ya leo ili;-

     1)Kujionea wenyewe madhara yaliyotokea
     2)Kutoa pole kwa waumini wetu
     3)Kushiriki pamoja uchungu wa madhara yaliyotupata
     4)Kuwepo kwa pamoja namna ya kukabiliana na uvamizi huo

Baada ya kutembelea maeneo yaliyovamiwa na kujionea uharibifu uliotokea:-
     1. Tumeona uchungu na masikitiko ya kwamba watanzania tumefikia
         kiwango hicho cha kumtendea jirani  yake 
    2. Tunatambua subira na uvumilivu mkubwa uliooneshwa na wakristo
        kuepusha majibizano ambayo yangeweza kuleta athari kubwa zaidi.
    3. Tumeziona juhudi za jeshi la polisi katika kudhibiti hali ya vurugu na
       kuepusha kupoteza uhai wa raia.

Katika wakati huu:- 

     1. Tunawaalika wakristo wote kutolea sala na maombi kwa Mungu aliye
         mlinzi wetu,usalama na ulinzi wetu uko mikononi mwa Mungu pekee.

     2. Tunatambua kuwa usalama wa wafuasi wa Kikristo ni haki ya msingi
         kama raia wengine wowote, ni mategemeo yetu kwamba wakristo na
        nyumba zao za ibada vinastahili kuhakikishiwa usalama.

Tunapenda kuwaambia Wakristo wenzetu kwamba kikao chetu cha leo kimetupa fursa ya kujionea wenyewe hali halisi ya uvamizi, kwasasa tunajiandaa kuchukua hatua muafaka. Tutawarudia hivi karibuni mbele ya vyombo husika yale yaliyo maamuzi yetu.

Kwa wakati huu tunawaomba muendelee kuwa wavumilivu na watulivu na muwe macho katika kulinda mali na nyumba zetu za ibada kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

Tunawapa pole wote na kuwatakia Baraka za Mungu.


Monday, October 15, 2012

TAMKO LA KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD, KUHUSU UCHOMAJI MOTO MAKANISA


Dr. Barnabas Mtokambali Askofu mkuu wa kanisa la TAG


Oktoba 12 mwaka huu, matukio mabaya na yenye kutia doa sifa ya amani umoja na Utengemano wa Taifa la Tanzania, yalijitokeza huko Mbagala Jijini Dar es Salaam, wakati watu wenye jazba wanaoaminika kuwa ni Waislamu wenye msimamo mkali walipovamia makanisa saba ...na kuyachoma moto eti kwa kulipiza kisasi cha mtoto aliyekojolea kuran katika utani wa kitoto
Katika mkasa huo ambao ni kama muendelezo wa ghasia zingine zilizotokea kule Zanzibar miezi michache iliyopita na kuteketeza makanisa mbalimbali mbali na kuharibu mali za kanisa na zile za watu binafsi.

Tukio la Mbagala limesababisha makanisa saba kuharibiwa vibaya, mali kuibiwa na hata kuhatarisha maisha ya watanzania na kuwafanya waishi kwa hofu na kupoteza matumaini. 

CHANZO CHA TUKIO

Kwa mujibu wa walioshuhudia, Polisi na wahusika (Waislamu) chanzo cha ghasia hizo na mabishano ya kitoto baina ya watoto wa dini ya Kiislamu na kikristo, waliobishana kuwa ikiwa mtu atakojolea kuran na kuitemea mate atageuka mbuzi au nyoka.

Lakini baada ya tukio hilo la kitoto watu walilikuza na kulipeleka kwenye misikiti na hivyo kuchocheza ghasia. Kimsingi tukio lenyewe ni jepesi sana ukilinganisha na matokeo yake. Ukweli kwamba waliofanya utani huo ni watoto na chanzo chake ni mabishano ya kitoto, unatia shaka kuwa huenda kuna hoja nyuma ya pazia ambayo isipotazamwa kwa makini inaweza kulete matokeo mabaya sana.
Jambo linalonitia shaka ni kufanana kwa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa ya Zanziabar na ya Mbagala ambapo hakukuwa na uhusiano wa vyanzo vya ghasia na makanisa husika.

Mfano; Ghasia za Zanzibar zilizopelekea kuangamizwa kwa makanisa zinaelezwa kuwa zilitokana na kikundi cha Kiislamu cha Uamsho wa Mihadhara, kilichokuwa kikiandamana kudai mjadala wa Muungano, lakini zikaishia kwenye uchomaji wa makanisa, hapa hauonekani uhusiano wa kanisa na Muungano; nalazimika kujiuliza kulikoni?
Vivyo hivyo tukio la Mbagala halina uhusiano wa moja kwa moja na kanisa kwa kuwa hakuna ushahidi wala hata tetesi kuwa mtoto huyo alitumwa na kanisa lolote. Wahusika wa dini ya Kiislamu akiwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, analielezea tukio la kitoto kama lisilostahili hata mtu kufunguliwa mashtaka bali kuelekezwa tu. Ni vipi lisababishe uchomaji wa makanisa?


MAKANISA YALIYOCHOMWA MOTO

Katika ghasia hizo za aina yake, makanisa saba yamethibitishwa kuharibiwa kwa kuchomwa moto, kupasuliwa vioo, viti na kuibiwa vyombo vya muziki na jenereta. Makanisa hayo ni TAG Kizuiani, Agape, Kibonde maji, SDA Sabato, Mbagala Kizuiani, Katoliki Kristo Mfalme Mbagala Rangi Tatu, Anglican Mbagala Kizuiani, KKKT, Mbagala Zakhem na TAG, Shimo la Mchanga.

Pamoja na majengo hayo kubomolewa kwa viwango tofauti mengine yakichomwa moto, pia wahusika waliiba Genereta, na vyombo vya muziki vya makanisa hayo na kuvunja magari na baadhi yao kuchomwa moto.

Choko choko zilizinazoweza kuwa cahanzo cha matukio hayo ni:
Januari sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKITA, kiliitisha kongamano la kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislamu. Katika kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kulitolewas kauli za kichozi kama:

1. Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2. Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3. Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4. Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.
Kauli hizo zilitolewa na Sheikh Nasoro Mohamed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.

Uchunguzi unaonesha kuwa uchochezi huu umekuwa ukiwaandaa watu kusubiri vijitukio vidogo tu ili kulipua ghasi. Tuliona jinsi makanisa yalivyochomwa kule Zanzibar. kwa kuwakumbusha tu makanisan yaliyoangamizwa katika tukio hilo ni: EAGT, Elimu Pentecost na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT.

Ni jambo la kusikitisha kuwa matukio haya yanatokea siku mbili tu kabla ya maadhimisho ya miaka 13, ya kifo cha Rais wa Kwanza, Mwl. Julius kambarege Nyerere. Leo hotuba na midahalo inarindima kila mahali kumuenzi Nyerere, lakini wengi wetu tukiwa tumejaa majozi baada ya nyumba zetu za ibada kuharibiwa katika matukio yanayoashiri hatari kubwa.
Hofu yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:

1. Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo 500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.

2. Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.

3. Itakumbukwa kuwa miezi michache tu ilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.

4. Katika tukio hilo inasemekana mtoto huyo alitengenezewa mabishano ya kitoto kuwa akichoma kurani atakuwa chizi naye akabisha kisha akapewa kiberiti na kurani akachoma tena walioandaa mzaha huo wakamkamata na kumpeleka mahakamani. Tukio linalofanana na hilo lilitokea tena Bagamoyo mkoani Pwani ambapo mtoto wa kike alishtakiwa na hata kuhukumiwa kifungo kwa madai ya kuchoma kuran lakini tukio lilikuwa katika mabishano ya midhaha ya kitoto

WITO WANGU

Natoa wito kwa Wakristo wote nchini kujiepusha na mizaha inayoweza kutengeneza sababu za kulipuka kwa ghasi na kutengeneza mwanya wa watu wenye nia mbaya kutekeleza agenda zao zaria Ili kulinda amani umoja na utengemano wetu, nawasihi viongozi wa makanisa kuonya na kukemea waumini na watoto wetu wasishiriki kwa namna yoyote ile mizaha inayopelekea kuchoma au kuharibu vitabu au nyaraka za kidini.

Nawasihi watanzania wote kwa ujula kujiepusha na mizaha ya kidini inayoweza kuchafua amani yetu, na pale jambo lolote lenye kukera linapotokea tujiepushe kuwa mawakala wa shetani wa kueneza chuki badala ya amani na upendo.


USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI 

Nawashauri viongozi wa Serikali ambao leo wanatoa matamko na kushiriki midahalo ya kumuenzi Mwl. Nyerere kukumbuka kuwa huyo alikuwa na mapenzi makubwa na amani na umoja wa taifa. Kwa hiyo kumuenzi kwa vitendo ni kudumisha utawala bora, unaofuata sheria usio na chembe ya ubaguzi wa aina yoyote.

Kulipuka majukwaani kumuenzi Nyerere bila kuilinda na kuitetea amani ya nchi ni kujidanganya.

Ni wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.

Viongozi wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.

Pia ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.

Ni vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta. 

Ni vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele zake.
Ni vyema viongozi wa Serikali wakajizuia kufanya maamuzi yanayoashiria upendeleo kwa baadhi ya makundi ya kidini na kukiuka utawala wa sheria, mfano; kutii waandamanaji na kuwaachia bila mashrti watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria kuna jenga kiburi kwa makundi yenye kiu ya matumizi ya nguvu na kujenga hofu kwa pande zingine.
Ni vyema mamlaka zikasiamama katika sheria na kufanya hukumu kulingana sheria badala ya kuamua mambo ya kisheria kisiasa.

WITO MAALUMU KWA VIONGOZI WA DINI

Nitumie nafasi hii kuwasihi vingozi wenzangu wa dini, kusimama imara katika kuombea taifa na kuhubiri kwa nguvu ili kukabiliana na giza la kiroho ambalo linatishia kuifunika nchi.
Takwimu za karibuni kabisa za utafiti uliofanywa na taasisi ya Washnton DC iitwayo, Pew Research Centre, na kurushwa na Televisheni ya CNN, Katika kipindi chake cha Inside Africa, zilionesha kuwa watanzania asilimia 93, wanaamini mambo ya ushirikina na uchawi wakati Uganda ni asilimia 29 na Kenya ni asilimia 27. Tu. Mahali ambapo giza la kiroho limezingira kiasi hiki ni lazima matukio ya kishetani yashamiri tuchukue hatua.

Mwisho, natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa letu, tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.

Imetolewa leo 14/10/2012
Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG


TUNAJIFUNZA NINI KWA YALIYOTOKEA MBAGALA?



Ndugu zangu watanzania, napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole Wakristo wote kwa yote yaliyotokea mbagala na kwa uharibifu mkubwa uliofanywa wa nyumba za ibada (makanisa). Najua inauma sana na imeleta usumbufu mkubwa sana miongoni mwetu. Mbali na yote namshukuru Mungu wa Bwana wetu Yesu atupae amani na subira hasa tunapopita katika matatizo makubwa kama haya. Ni maombi yangu kuwa, Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo aendelee kutupa amani, furaha na upendo kwa mapito yote tupitiayo.
Tunapoona haya yote yanatokea, naomba niwakumbushe wakristo wenzangu vitu kadhaa katika misingi na imani ya Kikristo;-

v  Kushindana kwetu sii juu ya damu na nyama bali ni katika falme na pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Waefeso 5).Huu ni wakati wa Kumwomba Mungu na wala si wakati wa kupambana na katika damu na nyama. Katika hali isiyoyakawaida, kuna vitu vingi sana vinaendelea katika ulimwengu wa roho(usioonekana). Unachokiona kinatokea au kinafanyika katika ulimwengu huu unaooneka kimeanzia katika ulimwengu unsioonekana (ulimwengu wa roho).Wakristo wanajua siri hii, hivyo ni wito wangu kwamba, twende katika maombi na tumwite Mungu, na tuharibu kila utendaji na hasa wimbi hili la uharibifu linaloendelea katika nchi yetu. Najua na nina uhakika kwamba litakoma katika jina la YESU.

v  Ukristo umejengwa katika msingi thabiti na imara ambao ni YESU mwenyewe. Yesu alikuja duniani  kumuokoa mwanadamu aliyekuwa amepotea katika dhambi ili amuweke katika ufalme wake. Katika harakati zake za kumuokoa mwanadamu, Yesu hakutumia upanga wala hakumwaga damu. Yesu aliwapenda na anawapenda watu wote. Anawapenda adui zake,na aliwaombea( Mathayo 6,7,8,9).Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na  wakristo wote duniani.Pamoja na yote yaliyotokea mbagala, na mabaya yote wanayotendewa wakristo, ni muhimu tukapata msaada wetu toka kwa Mungu. Kulipiza kisasi si juu yetu, Biblia inasema kisasi ni juu ya Mungu mwenyewe.

v  Kunajambo Mungu anasema na kanisa la Tanzania: wakati huu ambapo tumeshuhudia makisa saba (7) yakichomwa na Waislamu Dar es salaam, Mbagala na mengine yaliyochomwa Zanzibar, na Mwanza. Bila shaka Mungu anasema kitu, na anataka atufundishe kitu fulani.Ni maombi yangu kuwa Mungu aseme nasi,naomba kanisa la Mungu Tanzania, litege masikio yake lipate kusikia na kuona kile Mungu anafanya Tanzania.Hakuna kitu ambacho kinaweza kutendeka duniani pasipo Mungu kuwajulisha watumishi wake. Naomba wakristo wenzangu tumwombe Mungu, wako wapi wanawake waombolezaji, nawajitokeze sasa wakaomboleze juu ya Taifa la Tanzania, Juu ya wamama,watoto, wababa, wazee na vijana wa Tanzania.

v  Maombi na subira ndiyo silaha yetu: napenda niwakumbushe wakristo wenzangu kwamba,sisi tunajivunia maombi silaha yetu ya ushindi.Kwa mkristo yeyote na mahali popote alipo lazima atambue kuwa huu ni wakati wa maombi na wala si maneneo tu yasiyokuwa na tija. Kupitia maombi tunaweza kutuliza dhoruba na hali ikawa shwari. Namwamini Mungu anaweza kutuliza hali, na amani ikaendelea kudumu katika Taifa letu. Hii itawezekana tu endapo ufahamu huu utawaingia Wakristo na wakaingia kwenye maombi ya kudhamiria. 2 Nyakati 7:14) inasema ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu....................nitasikia toka juu mbinguni nitasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao.

Naomba niwasihi watanzania na wakristo wote Tanzania kuwa na subira na kumwachia Mungu awatetee katika yote wanayopitia.Hakuna mtu aliyeamua kumtegemea na kumwamini Mungu kwa dhati, halafu mwisho wa siku akaaibika au Mungu akamwacha mtu huyo, haiwezekani.
POLISI WAKIWASHIKA BAADHI YA WALIOSHIRKI KATIKA VURUGU

VITU VIKIWA VIMECHOMWA BARABARANI

MOJA LA GARI LA POLISI KATIKA KUWADHIBITI WAANDAMANAJI

POLISI WAKIDUMISHA USALAMA KATIKA ENEO LA TUKIO

MOJA KATI YA MAKANISA SABA LIKICHOMWA MOTO

WAISLAMU WAKIWA KITUO CHA POLISI WAKIDAI WAPEWE MTUHUMIWA WAO

MLANGO WA KANISA UKIWA UMEHARIBIWA KWA MAWE

WACHUNGAJI NA WAUMINI WAKIANGALIA UHARIBIFU ULIOFANYWA KANISANI

MABENCHI YA KANISA YAKIWA YAMEVUNJWA KABISA

MABENCHI YAKIWA YAMEVUNJWAVUNJWA

MIMBARI IKIONEKANA KUCHOMWA MOTO KABISA

HUU NI UHARIBIFU MKUBWA

BAADHI YA VYOMBO VYA MUZIKI VIKIWA VIMEUNGUZWA

MADIRISHA NA MILANGO IKIWA IMEHARIBIWA KABISA

OFISI YA MCHUNGAJI IKIWA IMEHARIBIWA KABISA

BAADHI YA WACHUNGAJI WAKISUBIRI TAARIFA KUTOKA POLISI

BAADHI YA WAUMINI WAKIOMBA MUNGU

VYOMBO VYA MUZIKI VIKIWA VIMECHOMWA MOTO

WAUMINI WAKITAFAKARI KILICHOTOKEA KANISANI KWAO

MOJAWAPO LA GARI LILILOHARIBIWA VIBAYA KABISA



KUSHOTO NI MSIKITI AMBAO WAISLAMU WALIJIKUSANYA NA KULIVAMIA KANISA UPANDE WA KULIA NA KUFANYA UHARIBIFU MKUBWA

Friday, October 12, 2012

UOVU HUONEKANAJE?



Vitu vingine huonekana na kusababisha hisia za woga, na kutahadharisha. Ebu chukua mfano wa nyoka. Kwa watu wengi, nyoka mara zote hubeba na kuonekana kama ishara ya uovu na hatari. Mimi binafsi siwapendi nyoka. Hutemebea taratibu kwa kujifuta ili wasisikiwe na watu. Kama ungeweza kuniuliza kwa nini, kuna sababu nyingi na nzuri hapa: macho yao madogo ya mduara, matendo/mwendo wao wa kitahadhari, mwendo wao usiogundulika kirahisi, ngozi zao nyororo na zenye utelezi(ndio, najua , magamba)… mwendo wao wa kiupandeupande, na mara zote huonekana wako tayari kushambulia yeyote mbele yao. Lakini kama mwendo na uhatari wao ndo unawafanya kuwa waovu, kwa nini isiwe papa, buibui au hata simba?
Naamini tunaweza kupata jibu zuri kutoka katika bustani za Edeni. Shetani, baada ya kumwasi Mungu na kufukuzwa mbunguni, alichagua kujificha kwa umbo la nyoka. Ikiwa ni matokeo, maelfu ya miaka baadae, bado tunahusisha nyoka na uovu kwa umbo lake la asili.
Nilikuwa nasoma kitabu cha Yakobo ghafula  nikamwelewa nyoka kwa njia ya tofauti sana, baada ya ufahamu ulionijia kwa mfano wa ubaya zaidi ya ulivyofafanuliwa. Kaika Sura ya 3, Yakobo anawahusia wakristo watambue umuhimu wa kuwa makini na maneno yao/kulinda ndimi zao. Alifafanua ulimi wa mwanadamu ni kama:
“...Haujatulia na muovul, umejaa sumu.” (Mstari wa 8)
Lakini unakuwa mbaya zaidi:
“Mara nyingine[ulimi] humsifu Bwana na Baba yetu, na mara zingine tunautumia kuwa laani wote walioumbwa kwa mfano wa Mungu.” (Mstari wa 9)
Je ulishafanya hivyo? Mimi najua nisha wahi kufanya hivyo.
“Na ndivyo baraka na laana zinatoka kwenye kinywa kimoja.” (Mstari wa  10a)
Mara baada ya kusoma mstari huo, sura ya ndimi mbili ndefu za nyoka nilizozitafakari katika mawazo yangu. Biblia inaeleza na kufafanua juu ya mahubiri mabaya kwa njia hii: “Usengenyaji, kuwadharau wengine, kujisifu, kuwanyanyasa wengine, walimu wa uongo, malalamiko na uongo.” Kwa bahati nzuri kila mtu anajua ni mara ngapi ameutumia ulimi wake vibaya akidhani kwamba Mungu hamuoni.
Ni rahisi sana kuufikiria uovu kama uasi, ukali, na wenye sumu kali. Shetani akiwa mwenye ghadhabu na hasira nyingi baada ya kufukuzwa mbinguni, alimwendea Adam na Hawa kwa umbo la Nyoka bila kuogopa. Kwa ujanja mwingi akitumia maneno mazuri yaliyojaa wingi wa ushawishi, huku akiwa amejaa hasira, kinyongo na wivu wa kutaka kumharibu na kumnyang’anya mwanadamu mamlaka aliyopewa na Mungu. Shetani alifanya kwa urahisi kabisa, hakutumia silaha ,uchawi, mazingaumbwe wala nguvu. Alichofanya shetani ni kidogo sana, alitumia silaha ndogo na inayodharauliwa na wengi, “ULIMI”. Kwa ulimi, Shetani aliweza kumjaribu Adam na Hawa kwa swali moja na rahisi,
“Eti Mungu amesema…” (Mwanzo 3:1b)
Kama wakristo, tunafanya kila iliyo juhudi kujilinda na aina zote za uovu. Mauaji, Uzinzi, wizi… lakini bado, tumeshindwa kugundua kwamba kinachotoka vinywani mwetu vinauwezo mkubwa wa kutuletea maumivu, kutujeruhi…na ndiyo, hata kifo.
“Chochote kiujazacho moyo wako ndicho ukisemacho…kwa sababu ndani ya moyo wa mwanadamu hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, aina zote za uasherati, wizi, usengenyaji, na  uongo.” (Mathayo 12:34, 15:18-19)
Tunajilindaje wenyewe na  “umbea, kuwadharau wengine, na walimu wa uongona uongo?” Biblia inasema juu ya yote,
“Linda sana moyo wako, maana ndiko zitokako chemichemi za uzima.” (Mithali 4:23) 
Swali linabakia, Je mtu anawezaje kuulinda moyo wake? Ni kwa kuyakumbuka na kuyatenda yote aliyoyaamuru Mungu na kwa kuwa tayari kufunikwa na nguvu za nane lake kinyume na mipango miovu ya shetani,
“Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi.” (Zaburi 119:11)