Friday, March 23, 2012

WOKOVU

Wokovu ni mpango wa MUNGU kumkomboa/Kumtafuta mwanadamu kutoka katika maisha ya dhambi.Matendo ya mitume 17:30; Biblia inasema kwamba Nyakati za ujinga MUNGU alijifanya hazioni lakini sasa anaagiza watu wote watubu na kumrudia YEYE.Hakuna kitu kinacho mchukiza Mungu kama Dhambi.Toka mwanzo Mungu alimuumba mwanadamu tena kwa sura yake akiwa katika hali ya utakatifu, Lakini mwanadamu akafanya yaliyo machukizo mbele za MUNGU. Dhambi iliingia duniani kwa mara ya kwanza kupitia Adamu katika bustani ya edeni, baada ya MUNGU kumwambia Adamu kwamba matunda yote ya Bustani hii waweza kula ila usile matunda ya mti ulioko katikati ya bustani.Adamu alimwasi MUNGU baada ya kudanganywa na shetani hivyo alivunja amri ya MUNGU na akala matunda ya mti ule.
Toka dhambi imeingia dunia imeleta maafa na mapigo makubwa katika dunia yetu, Familia nyingi zimefarakana,Ndoa kuvunjika,Hakuna amani kati ya ndugu na hata taifa na laana imeila dunia.Na ashukuriwe MUNGU muumba mbingu na nchi kwa kutuletea YESU KRISTO kuwa mwokozi wa maisha yetu.Kuna uwezekano wa mtu kuponywa maisha, na hata kuimarishwa kwa mahusiano kupitia YESU. Hivyo mtu yeyote akimkiri YESU kwa kinywa chake na kuamini Moyoni mwake hakika ataokoka. YESU yupo na Wokovu upo pia, ni wewe tu kuamua leo hakika maisha yako yatabadilika na hakika utaishinda dhambi.
MUNGU akibariki sana.

No comments:

Post a Comment